Jumla
ya Wafungwa 293 kutoka magereza Ya Ukonga, Keko,Segerea na Wazo Hill
jijini Dar es salaam leo wameachiwa huru kwa Msamaha wa Rais wa Tanzania
Dkt. John Magufuli alietoa Msamaha kwa Wafungwa 5,533 waliokuwa
wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali Nchi nzima.

Wafungwa
hao wameachiliwa huru leo Mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es
salaam Bw. Abubakar Kunenge, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
salaam Lazaro Mambosasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam ambapo
kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha wa Rais
kuhakikisha hawarudii kufanya makosa.

Kwa
mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Kamishina Msaidizi wa
Magereza Julius Mtambala amesema kati ya Wafungwa hao 293 walioachiliwa
huru 130 wanatoka Gereza la Ukonga,54 Gereza la Keko, 74 Gereza la
Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo hill.