Wageni mbalimbali kutoka nchi za sadc watembelea banda la (msd) katika mkutano wa mawaziri wa afya

Bw. Marco Masala Meneja Manunuzi
Bohari ya Dawa (MSD) kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya (SADC) akitoa
maelezo kwa Beatrice Kasakati wa Malawi na Thenisi Gawa kutoka Mbabane
Eswatini  wageni waliotembelea katika banda la taasisi hiyo kwenye
maonesho kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa SADC
unaofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es
salaam
Beatrice Kasakati wa Malawi moja
wa maofisa wanaohudhuria katika Mkutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa
(SADC) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Bohari ya Dawa MSD
wakati alipotembelea banda hilo.
Thenisi Gawa kutoka Mbabane
Eswatini akisaini kitabu cha wageni katika banda la Bohari ya Dawa (MSD)
wakati alipotembelea katika banda hilo.

Beatrice Kasakati wa Malawi na
Thenisi Gawa kutoka Mbabane Eswatini  wageni waliotembelea katika banda
la taasisi hiyo kwenye maonesho kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na
Ukimwi wa (SADC) unaofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) jijini Dar es salaam wakimsikiliza Bw. Marco Masala Meneja
Manunuzi Bohari ya Dawa (MSD) kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya (SADC)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *