Waitara awaonya watakaofanya udanganyifu mitihani ya kidato cha nne

SERIKALI
imetoa onyo kwa wale wote watakaojaribu kufanya vitendo vya udanganyifu
kwenye mitihani ya kidato cha nne inayoanza kesho.Onyo
hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe
Mwita Waitara alipokua akitoa salami zake za heri kwa wanafunzi zaidi ya
Laki Nne wanaotarajiwa kumaliza mitihani yao ya kidato cha nne.Mhe
Waitara amewapongeza wanafunzi hao kwa uvumilivu wao kwa kipindi chote
walichokua shuleni na kuwataka kufanya vizuri mitihani hiyo ili kumpa
sifa Rais Dk John Magufuli kwa kutoa elimu bila malipo.Amesema
kumekuepo na vitendo vya udanganyifu kwenye vipindi vya mitihani ya
Kitaifa na kuwataka wazazi na wanafunzi kutodanganyika na kushiriki
vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na sheria.
Niwapongeze Wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani hii, Sisi kama
Serikali tunawatakia kila la heri, wakamtangulize Mwenyezi Mungu na
kuzingatia yale yote ambayo wamefundishwa kwa miaka minne.Lakini
pia niwasihi Walimu, Wazazi na Wanafunzi kutojaribu kushiriki vitendo
hivi kwa kununua mitihani kutoka kwa watu ambao wamekua wakiwalaghai
kwamba wanauza mitihani. Kufanya hivyo ni kujihatarisha kwani Serikali
iko makini na tukiwabaini tutawafutia mitihani,* Amesema Mhe Waitara.Amesema
tayari wameshatoa maelekezo kwa vyombo vya usalama kuwachukulia hatua
za kisheria wale wote watakaokutwa wakifanya udanganyifu huo kwani hauna
tofauti yoyote na rushwa na wizi.Waitara
pia amezungumzia mafanikio ya elimu bure ambapo wanafunzi hawa wa
kidato cha nne ndio zao la kwanza la elimu bure na kusema Serikali
itaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu na kutatua changamoto
zote ambazo zipo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira bora ya wanafunzi
pamoja na walimu.” Toka
Rais atangaze elimu bila malipo hawa ndio wanafunzi wa kwanza ambao
wanamaliza wakiwa wamesoma miaka minne bila malipo. Kwetu sisi ni
mafanikio makubwa kuona ndoto ya Rais Magufuli ya kupambana na ujinga
ikifanikiwa kwa kasi. Serikali
imekua ikitenga zaidi ya Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya elimu bure,
lakini pia kuonesha mafanikio yao idadi ya wanafunzi wanaomaliza mwaka
huu ni kubwa kulinganisha na ya mwaka jana. Mwaka huu wanafunzi
waliosajiliwa na wanatarajiwa kufanya mitihani ni 485,000 ambapo mwaka
jana waliofanya mitihani ni 427,000,” Amesema Mhe Waitara.


Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mwita Waitara akizungumza na
wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana na mitihani ya
kidato cha nne itakayoanza kesho.