MKUU
wa wilaya ya Karagwe Mhe Godfrey Mheluka kushoto ambaye alimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Kagera akikabidhi Cheti cha Utambuzi cha Mhe Mbunge
Neema Lugangira kwa Katibu wake Kitaifa Judith John leo
WALIMU Wanawake wakikabidhi kitenge kilichoandikwa “Super Woman”cha Mhe Neema Lugangira kwa Katibu wake Kitaifa Judith John
CHETI cha Utambuzi na Kitenge cha Super Woman alichopewa Mhe Neema Lugangira na Walimu wa Wanawake wa Bukoba Manispaa
Hivi ndivyo Cheti cha Utambuzi cha Mhe Neema Lugangira kilivyokuwa kinaonekana mara baada ya kukabidhiwa
Wanawake wa Manispaa ya Bukoba kupitia kitengo cha walimu Wanawake cha
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamemkabidhi Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira cheti cha Utambuzi na Sare ya Kitenge
kilichoandikwa “Super Woman”.
hicho ambacho kimekabidhiwa leo ikiwa ni siku ya Wanawake Duniani 2021
kinadhihirisha namna walimu hao wanavyothamini juhudi kubwa ambazo
zimekuwa zikifanywa na Mbunge Neema Lugangira katika kuchangia Maendeleo
ya Jamii wilaya ya Bukoba Mjini.
cheti hicho kwa niaba ya Mbunge Neema Lugangira ambaye yupo mjini
Dodoma kwa ajili ya Vikao vya Kamati za Bunge,Katibu wa Mbunge huyo
Kitaifa Judith John alisema kwamba cheti hizo wamekipata wakati muafaka
kutokana na juhudi kubwa zinazonyeshwa na mbunge huyo katika kuhakikisha
anawapa maendeleo.
cheti hicho,Mbunge Neema Lugangira aliwashukuru Walimu Wanawake wa
Manispaa ya Bukoba kupitia Kitengo cha Walimu Wanawake cha Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) Bukoba Manispaa kwa kutambua juhudi zangu za
kuchangia Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bukoba Mjini .
kweli kitendo hiki cha Walimu hapa kunipa Cheti cha Utambuzi na Sare ya
Kitenge iliyoandikwa “Super Woman” leo Siku ya Wanawake Duniani 2021
kinaonyesha namna wanavyotambua na kuthamini mchango wangu kwao na
nihaidi tutaendelea kushirikiana kuhakikisha wanapata mafanikio
makubwa”Alisema .
hivyo pia alimshukuru Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mhe
Godfrey Mheluka aliyekuwamwakilisha Mhe Mkuu wa Mkoa Kagera kwa
kumpongeza Mbunge Neema Lugangira na Shirika la Agri Thamani ambalo yeye
ni Mkurugenzi kwa namna ambavyo wameendelea kutoa Elimu ya Lishe Bora.
Neema aliongeza pia Mkuu huyo wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa
aliwataka waendeleze mapambano kwani Mkoa wa Kagera bado unaongoza kwa
idadi halisia kwenye Udumavu
Lishe hakuna Maendeleo na sisi tunakubaliana naye kabisa hivyo
tutahakikisha tunawaunga mkono walimu wote kwa lengo la kuhakikisha
tunaondokana na hali hii kuanzia shuleni hadi kwenye jamii”, Alisema
hivyo aliwashukuru Walimu Wanawake wa Bukoba Manispaa kwa Utambuzi huo
na anawasaidi huku akihaidi kushirikiana nao katika maeneo mbalimbali
hususan katika kufanikisha Lishe Shuleni na Hedhi Salama Shuleni