Walimu mkoani kagera watakiwa kuwa mabalozi wazuri wa a kulipa kodi ili kukuza uchumi wa nchi.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.

Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti  amewataka walimu
mkoani humo kuwa mabalozi wazuri kwa kulipa kodi ili kuweza kuchangia
ukuaji wa pato la nchi.
 
Mkuu
wa Mkoa Gaguti amesema hayo Septemba 23, 2019 wakati akifungua
kongamano la Walimu na Benki ya NMB Bukoba katika siku ya walimu kwenye
ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba .
 
Ameongeza
kwamba walimu  ni  jeshi kubwa kila watakapo kuwa wenasimama waendelee
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ulipaji kodi na kuwahamasisha wananchi
kudai risiti kila wakinunua bidhaa na kuwahamasisha wanaouza kutoa
risiti.
 
Mkuu
wa Mkoa Gaguti ametoa rai kwa benki ya NMB kuona namna ya kuwapunguzia
riba walimu sababu ni wadau wakubwa wa benki hiyo tangu mwanzo.
 
 Pia
amewataka walimu kutanua wigo wa kuunda vikundi vya pamoja mfano kwenye
Kata na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato
vyao hasa pale wanapostaafu. 
 
 Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Gabulanga iliyopo wilayani
Missenyi bwana Mutalemwa Makwabe kwa niaba ya Walimu wenzake amesema
kuwa wanaishukuru benki hiyo kwa namna inavyoendelea kuwajali walimu
pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika shule uku akitaja kuwa shule
yake iliwahi kupatiwa misaada mbali mbali na benki hiyo ikiweno madawati
pamoja na mbao za kuezekea.

Kwa
upande wake Meneja wa NMB kanda ya ziwa bwana Ibrahimu Agustino amesema
kuwa benki hiyo inatenga 1% kila mwaka katika kuhudumia jamii  na
kuongeza kuwa kwa mwaka huu wametenga shilingi bilioni moja na mpaka
sasa wametoa zaidi ya milioni mia sita katika  kusaidia jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *