Waliovunja bar na kuiba k vant wafikishwa mahakamani kahama

Na Salvatory Ntandu – Malunde 1 blog Kahama 

Wakazi
wawili wa Mtaa wa Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Meshaki
Joakimu (31) na Godfrey Luka (32) wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya
ya Kahama kwa tuhuma ya kuvunja baa(grocery) na kuiba fedha, na thamani
mbalimbali za ndani pamoja na vinjwaji  Mali ya Eliasi Mwasenga.


Akisoma
Shauri hilo Januari 14 mwaka huu mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi
Felix Mbisse mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidi wa Mahakama hiyo Evodia
Kyaruzi amedai watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 8 mwaka 2019
usiku majira ya saa nane usiku.

Alisema
kuwa baada ya kuvunja baa hiyo waliiba Televisheni mbili,bia kreti
5,konyagi chupa 10,K vant chupa 10,flash disck mmoja vyote kwa pamoja
vikiwa na thamani ya shilingi milioni mmoja laki sita na elfu ishirini
mali ya Eliasi Mwasenga.

Katika
shauri hilo la jinai namba 10 la mwaka huu Mbisse alisema kuwa wawili
hao kwa pamoja wanatuhumiwa kutenda makosa mawili ambapo kosa la kwanza
ni la kuvunja nyumba kinyume na kifungu 296 cha kanuni ya adhabu sura 16
marejeo ya mwaka 2002.

Shitaka
la pili wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuiba mali hizo kinyume na kifungu
cha 258 (1) na 265 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka
2002.

Washitakiwa
wote kwa pamoja walikana kutenda makosa hayo na Shauri hilo
limeahirishwa hadi Januari 24 mwaka huu na wameachiliwa huru kwa dhamana
baada ya kutimiza mashariti yake ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini
wawili wawili ambao walisaini bondi ya shilingi milioni mmmoja kila
mmoja.