Wamiliki wa viwanda watakiwa kutoa kushirikiano ofisi ya taifa ya takwimu

Na: Mwandishi Wetu
Wamiliki
wa Viwanda nchini wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kukuza sekta hiyo ambayo imekuwa ni chachu
ya maendeleo kwa Taifa.Maagizo
hayo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
(Mb) alipokuwa akifungua Mkutano wa Tatu wa wa Baraza la Tano la
Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo alipokea taarifa ya
changamoto ambazo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekuwa ikikabiliana
nazo ikwemo suala la wenye viwanda kutokutoa ushirikiano wakati ofisi
hiyo inapokusanya takwimu viwandani.

Waziri
Mhagama alieleza kuwa Serikali imejiwekea mikakati maalumu katika
kukuza sekta ya viwanda, ili kufikia maendeleo ya sekta hiyo taarifa
sahihi zenye takwimu zilizochakatwa ni muhimu zikawepo katika kufanya
maamuzi stahiki na kupanga mikakati ya maendeleo.

“Ili
kufikia lengo la kuinua uchumi wa nchi, ni muhimu wenye viwanda
wakatambua umuhimu wa uwepo wa takwimu sahihi ambazo zitaleta tija na
ustawi wa sekta hiyo na hayo yamejidhihirisha hasa kupitia dhamira ya
Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kukuza uchumi wa
nchi kupitia viwanda,” alieleza Mhagama

Aliongeza
kuwa uwepo wa ushirikiano huo utaleta tija na ustawi wa sekta hiyo
kutokana na upatikanaji wa taarifa za takwimu mbalimbali kuhusina na
viwanda vilivyopo nchini ikiwemo tafiti za uzalishaji wa viwanda, kujua
masula ya ajira, ujuzi ambao haupo nchini na umekuwa ukitoa ajira kwa
wageni wa nje na pia kujua mahusiano ya ukuaji wa uchumi na sheria za
kazi zinavyoshahabiana.

Sambamba
hayo Waziri Mhagama ametoa maagizo kwa Kamishana wa Kazi kuhakikisha
anashirikiana na kuwahusisha wataalamu wa takwimu wanapokuwa wanafanya
kaguzi kwenye viwanda mbalimbali hapa nchi ili takwimu zitakazokuwa
zinahitajika ziweze kupatina.

 “Jukumu
kubwa mlilonalo wakati huu ni kuwapatia elimu ili watambue umuhimu wa
kuwepo kwa takwimu za sekta hiyo na baada yah apo watakuwa na uelewa
kuwa ni wajibu wao kutekeleza suala hilo kisheria,” alisema Mhagama

Naye
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa alieleza kuwa ushirikiano
utakao kuwepo baina ya wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idara
ya Kazi na Wizara ya Viwanda na Biashara utasaidia kuimarisha njia bora
ya ukusanyaji wa takwimu za sekta hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *