Wanaccm watakiwa kuwaonyesha upinzani mahaba na kutotengeneza maadui

madiwani waliorudi ndani ya CCM kutoka Chadema wakicheza mara baada ya kula kiapo cha
Mwanachama wa CCM mbele ya Katibu wa siasa na uhusiano wa Kimataifa
Ngemela Lubinga kwenye maadhimisho ya miaka 43 ya chama cha Mapinduzi
sherehe zilizofanyika uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid Jijini Hapa
picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
wabunge wa mkoa wa Arusha Julius Kalanga Monduli,Katherine Magige viti
Maalum,Stephen Kiruswa Longido na James Ole Milya Simanjiro picha na
Ahmed Mahmoud Arusha.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akiongea na wanachama
wananchi na wapenzi wa chama hicho mkoa wa Arusha kwenye viwanja vya
Sheikh Amri Kaluta Abeid Jijini Hapa picha na Ahmed Mahmoud Arush
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wananchi na
wanachama wa CCM wametakiwa kutotengeneza Maadui na kuishi nao vizuri
kwa ushirikiano ili kuwaonyesha CCM iliyo imara.
Kwa
muktadha huo Tujihadhari na Maadui wa nje na ndani ambao wanataka
kutufanya tugombane ili waweze kuuza silaha kwa kuwa wamoja na kujenga
mashikamano ndani yetu.
Kauli
hiyo imetolewa na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga wakati akihutubia
kwenye sherehe za miaka 43 ya chama cha Mapinduzi kwenye uwanja wa
sheikh Amri Abeid Jijini Hapa na kuwataka wananchi kutunza siri za nchi
zitakazo saidia kupambana na Maadui zetu.
Aliwaonya
wanachama wa chama hicho kutofanya kampeni mapema na kusubiria muda
utakapofika kwa chama hicho kinautaratibu wake iliojiwekea.
Alisema
kuwa chama hicho kinajitegemea wala hakiombi fedha kutoka kwa wahisani
kwa kuwa mapato yameongezeka kutoka bilion 30 hadi takribani bilion 900
na kina fedha za kushiriki uchaguzi bila kuomba msaada.
“Niwasihi
wanachama wenzangu kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati kwa kuwa
chama chetu kina utaratibu wake” alisisitiza Kanali Ngemela.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa mkoa huo Zeletho Stephen alisema kuwa chama
hicho mkoa wa Arusha hakitarudia makosa ya mwaka 2015 na kuahidi ushindi
kwenye uchaguzi wa mwaka huu siku ikifika.
Akawataka
wanachama wa.chama hicho kujenga chama na kujitoa kwa nguvu kuhakikisha
chama hicho kinapata ushindi na kutuma salamu kwa mh.Raisi kuwa
wanachama wa chama hicho hawatarudia kosa walilolifanya huko nyuma.