Wanafunzi 900 wa kidato cha tano na sita mkoani tabora wapigwa msasa kuhusu sekta ya angaa na tcaa

NA TIGANYA VINCENT

JUMLA
ya wanafunzi 900 wa Kidato cha Tano na Sita mchepuo wa Sayansi katika
shule za sekondari tatu za Mkoani Tabora wamepewa elimu juu ya kujiunga
na sekta ya usafiri wa Anga pindi watakapoliza shahada zao za vyuo vikuu
katika fani za Sayansi.

Mafunzo
hayo ya siku moja yamehusisha wanafunzi 500 wa Shule ya Sekondari ya
Milambo, 200 WA Tabora Wavulana  na 200  wa Tabora wasichana.

Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Tabora mara baada ya mafunzo hayo,
Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini(TCAA)  Bestina Magutu
alisema lengo la elimu hiyo ni kuwasaidia wanafunzi wanasoma masomo ya
sayansi kuwa na uelewa mpana na kuchangamkia fursa ya masomo yanayohusu
sekta ya anga.

Alisema
lengo jingine ni kuwahamasisha ili waanze kujiandaa kwa ajili kusomea
fani mbalimbali za sekta ya anga kama vile urubani , uongozaji ndege,
ufundi wa ndege , usimamizi wa usalama wa usafiri wa anga na huduma kwa
wateja.

Kwa
upande wa Mkufunzi kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga Thamarat Salim
alisema sekta ya usafiri wa Anga hapa nchini inakuwa kwa kasi ni vema
wanafunzi wanasoma masomo ya sayansi wakachangamkia fursa hiyo kwa ajili
ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuelekea uchumi wa Kati.

Alisema
kozi nyingi za sekta ya usafiri wa anga zinamtaka mwanafunzi anayetaka
kusomea kozi hizo ni vema awe amesoma masomo ya sayansi.

Naye
Mwalimu kutoka Shule ya Sekondari ya Milambo Euphrahim Daffa alisema
mafunzo yanayotolewa na TCAA kwa wanafunzi wanachukua masomo ya sayansi
yamesaidia kuwaelimu sio tu wanafunzi hata walimu ya kujua kuwa hata
wanafunzi anayechukua Fizikia ,Kemia na  Bioloji ( PCB) anaweza kujiunga
na kozi za sekta ya anga.

Alisema
hatua imesaidia kuwafumbua macho na kutambua kuwa kusoma PCB sio tu
atasomea masomo ya sekta ya afya na  kilimo au walimu pekee yake bali 
hata sekta ya anga wanayofursa.

Meneja
wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  nchini Mkoa wa Tabora Daniel Nyimbo
alitoa wito kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kuchangamkia fursa
ya masomo hayo usafiri wa anga pindi zinapotangazwa katika vyombo vya
habari mbalimbali hapa nchini.

Alisema
kumekuwepo na fursa za kupata ufadhili wa kusomeshwa na TCAA kupitia
kufanya usahili na pindi wanaposhindwa kusomeshwa kwenye kozi mbalimbali
na kusema kuwa wanapoona hivyo wameombe.

TCAA
inaendelea na utoaji wa elimu ya sekta ya anga kwa ajili ya
kuwahamasisha wanafunzi wengi kusoma masomo ya sayansi kwa ajili ya
kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi wa Kati ambao
msingi wake mkubwa ni viwanda.

MWISHO