Wanafunzi shinyanga watakiwa kuweka bidii, juhudi na maarifa kwenye masomo yao

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Katibu msaidizi
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele, amewataka  wanafunzi kuweka bidii,juhudi na maarifa
kwenye masomo, kama hatua ya kukabiliana na ushindani katika soko la Elimu na  ajira

Akizungumza na
wanafunzi wa klabu ya maadili katika shule ya Sekondari Uhuru na Town  Shule ya Msingi zilizopo katika Manispaa  ya Shinyanga, ambapo amewataka kuepuka tama na
vishawishi.

Mwaitebele
amewasisitiza wanafunzi hao kujitunza na kujilinda dhidi ya mazingira hatarishi
yanayoweza kuwasababishia kufanyiwa ukatili wa kijinsia

Kwa upande wake  mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga
Bwana Bakari Kasinyo amewataka wanafunzi hao kuzingatia uadilifu ili waweze kuhitimu
masomo yao salama.

Baadhi ya wanafunzi wa
klabu ya maadili katika shule za sekondari Uhuru  na Town shule ya msingi wameahidi kusoma kwa
bidii huku wakieleza umuhimu wa klabu ya maadili shuleni.

Viongozi wa klabu ya
maadili kanda ya magharibi na viongozi wa klabu ya Mkoa wa Shinyanga
wametembelea baadhi ya Shule zenye klabu ya maadili katika Manispaa ya
Shinyanga ikiwemo Shule ya sekondari Uhuru, shule ya msingi Town pamoja na
shule ya Msingi Jomu.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele akizungumza.Wanafunzi shule ya sekondari Uhuru.

Picha ya pamoja katika shule ya msingi Town