Egidia Vedasto
APC Media, Arusha.
Wananchi jijini arusha wamejitokeza kwa wingi katika maombi maalum yaliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9 1961.
Wakati akizindua maandamano hayo ya amani ya kuuombea mkoa na taifa, Makonda amesema ni vema wananchi kudumu katika maombi ili kupigana vita na wanaliwazia kinyume taifa.
Maombi hayo maalum yamehudhuriwa na Vion gozi wa madhehebu na dini zote na kutoa maneno ya baraka kwa wananchi.
“Maombi haya si ya kutembea tu, kuimba wala kupiga tarumbeta, bali ni maombi ya kujikomboa, kurudisha kilichochukuliwa na kupigania kesho yetu iliyo nzuri, lazima tudumu katika maombi ili pamoja na familia zetu tukae vizuri”,
“Mimi ni mkuu wa mkoa lakini bila maombi siwezi kwenda, je wewe ambaye hata si mwenyekiti wa mtaa kwa nini usiombe? tusinyamaze tutembee tukiomba ili Mungu afanye kitu katika maisha yetu” amesema Makonda.
Aidha amesisitiza kuombea watoto ili kuondoa laana za mababu ambazo kwa kiasi kikubwa, zimefanya watoto wamechanganyikiwa na kuharibikiwa baada ya wazazi wengi kuacha kutekeleza mila.
Kwa upande wa Shekhe wa Mkoa Shaban Juma na Mchungaji Israel Maasa wamesisitiza watanzania kuombea nchi ili amani idumishwe, ulinzi na usalama kwa viongozi wa kitaifa hata kwenye mitaa.
“Yatupasa kuomba wanawake kwa wanaume ili Mwenyezi Mungu atuondolee maafa na vurugu katika watu wetu, tunamshukuru Mungu aliyekuleta hapa kwetu mkuu wetu wa mkoa, maana ana sababu njema na sisi kwa sababu wewe ni mtu wa Mungu” wamesema viongozi wa dini.
Kwa upande wake Esta Munishi aliyehudhuria
maadhimisho hayo, amepongeza hatua hiyo ya kuliombea taifa, kwamba maombi yasikome bali yaendelee hususan kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
“Niliposikia maombi ya kuliombea taifa nilifurahi sana, mimi ni mtu wa maombi hata sasa nimefunga na leo ni siku ya saba, naamini Mungu atatenda mambo makubwa katika nchi yetu, hatatuacha na hataruhusu vita wala kumwagika damu kwa watu wake” amesema Esta.
“Natamani huyu kiongozi wetu mkuu wa mkoa adumu kwetu na awe anaitisha maombi ya mara kwa mara tuko tayari na tutafunga na kuomba.