Wananchi wilayani karagwe wapatiwa elimu ya ubora wa viwango vya bidhaa na chakula

 

Afisa udhibiti ubora, Mhandisi
Emmanuel Shilinde (TBS) akimweleze mfanyabiashara wa duka umuhimu wa
kusoma taarifa katika vifungashio na kununua bidhaa zilizothibitishwa
ubora wake na TBS kwa mfanyabiashara wa mikate wa eneo la Kayanga mjini,
wilayani Karagwe mkoa wa Kagera. Afisa
udhibiti ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS) akiwaelezea muuzaji wa
vyakula umuhimu wa kusoma taarifa katika vifungashio na kuuza bidhaa
zilizothibitishwa ubora wake na TBS kwa wafanyabiashara wa mikate wa
eneo la Omuroshaka, wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.

Diwani wa kata ya Bugene wilayani
Karagwe-Kagera Mhe. Mugisha Mathias akizungumza mara baada kukutana na
maafisa wa TBS baada ya kutembelea katika kata hiyo wakati wa kampeni ya
elimu kwa umma katika ngazi ya wilaya iliyokuwa inafanyika kanda ya
ziwa,Diwani
wa kata ya Bugene wilayani Karagwe-Kagera Mhe. Mugisha Mathias akiwana
baadhi ya viongozi wa kata hiyo wakipata picha ya pamoja na baadhi ya
maafisa wa TBS

Wanafunzi
wa shule ya msingi Kayanga na Rumanyika, wilayani Karagwe- Kagera
wakisikiliza kwa makini elimu ya viwango kutoka kwa Afisa masoko
mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka ili wawe mabalozi wazuri wa
masuala ya viwango katika kaya zao kwa miaka ijayo.

 

Wanafunzi wa shule ya sekondari
Bugene, wilayani Karagwe- Kagera wakisikiliza kwa makini elimu ya
viwango kutoka kwa maafisa wa TBS ili wawe mabalozi wazuri wa masuala ya
viwango katika jamii zao.

Shirika la Viwango Tanzania TBS
limeendelea na zoezi lake la kutoa elimu ya viwango vya ubora wa bidhaa
na Chakula kwa wafanyabiashara, mashuleni pamoja na wananchi kwa ujumla
wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Diwani wa kata ya Bugene wilayani
Karagwe Mhe.Mugisha Mathias ameipongeza TBS kwa elimu ambayo wanaitoa
katika wilaya hiyo kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara na wananchi kwa
ujumla hawakuwa na elimu ya ubora wa bidhaa kwa undani zaidi.

“Naipongeza TBS kwa kazi nzuri wanaoifanya na natoa wito waendelee na kasi hiyohiyo ya utendaji”. Amesema Mhe. Mathias.