Wanawake tabora watumia ugoro kupunguza hamu ya tendo la ndoa

Tumbaku inayoelezwa kutumiwa na wanawake mkoani Tabora kuweka katika sehemu zao za siri ili kumaliza hamu ya tendo la ndoa pindi wanapokosa huduma hiyo

Waswahili husema ukistaajabu ya musa utaona ya Firauni, Je unajua
matumizi yote ya tumbaku?

Mkoani Tabora nchini Tanzania
wanawake wamekua wakitumia Tumbaku ili kupunguza hamu ya tendo la ndoa. Huweka
sehemu ya siri kisha kuitoa baada ya muda.

Tabia hiyo imezoeleka sana miongoni
mwa wanawake wasio na wenza wao, ikiwemo wajane. Lakini kwa upande wa afya,
wako salama?

Wanawake hususani wasio kuwa katika
uhusiano na wanaume ama kuolewa hutumia njia kumaliza hamu zao.

”Mimi ni mjane, natumia tumbaku
katika kumaliza hamu zangu kwasababu sina mwanaume na wala sitaki mwanaume
mwingine, kwa wiki naweka mara mbili” anasema Zaituni shabani mmoja ya
wanawake wanaotumia tumbaku sehemu za siri.

Wanawake wengine nilizunguma nao
kama asha, si jina lake halisi anasema kuwa anatumia tumbaku kwasababu
alikimbiwa na mwanaume wakati ana ujauzito.

” kwakeli sitaki kusikia tena
wanaume mi nitabaki na tumbaku, mana nikitumia hamu yote inaisha sina haja
tena” anasema asha

Wanawake wote niliozunguma nao
wanakiri kuwa matumizi ya tumbaku sehemu za siri huwasaidia kumaliza hamu ya
tendo la ndoa.

TUMBAKU INATUMIWA VIPI SEHEMU ZA
SIRI?

Kwa mujibu wa wanawake hawa
huchukua majani makavu ya tumbaku kisha kutangwa na baada ya hapo huchanganya
na mafuta kidogo pamoja na magadi, ama na mara nyingine hutumia ugoro kufanya
mchangayiko huo. Baada ya hapo huweka sehemu za siri na kisha hupata muwasho
ambao ndio humaliza haja ya tendo la ndoa.

” mi huwa napaka mara mbili kwa
wiki na huwa naweka kwa muda kidogo kabla niondoe na kisha napata muwasho, na
wala sipati maumivu yoyote nikimaliza matamanio yangu ya kufanya tendo la ndoa
yanakua yameisha” anasema zaituni.

Kwa kawaida wanawake hawa baada ya
kupaka tumbaku ama ugoro sehemu za siri husikia kama wamekutana kimwili na
wanaume.
 Wanawake hawana uelewa wa kutosha kuhusu athari za tumbaku

WANAUME WANASEMA NINI?

Katika kijiji cha ugala suala hili
ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake lakini kwa upande wa wanaume si wengi
wanajua , na wanaojua wanasema kuwa imekua siri baina ya wanawake.

“Mimi nimekua nikisia lakini
mara nyingi ni kwa bahati mbaya wao wakiongea, na nikuwaliza , wanasema ni siri
yao ni baina ya wanawake na si wanaume”. Anasema mzee Usantu mmoja wa
wakazi wa kijiji cha Ugala.

KUNA ATHARI ZOZOTE KIAFYA?

Kwa mujibu wa baadhi ya wanawake
wanaotumia tumbaku sehemu zao za siri, wanasema hawajawahi kupata tatizo lolote
kiafya.

Lakini mtaalamu wa magonjwa ya
akina mama anasema kuwa baadhi ya wanawake wanaokutwa na viashiria vya saratani
hasa ya kizazi wamekua na historia ya kutumia tumbaku sehemu za siri

“Hatuna utafiti wa moja kwa
moja lakini data za kwetu hapa wakati tunawahoji tabia za mazoea walizonazo
baadhi wamekiri kutumia tumbaku , hivyo hiyo inaweza kuwa miongoni mwa sababu
na kama viashiria vingine vikiwepo” anasema daktari.

Matumizi haya ya tumbaku kwa
asilimia kubwa yamechangiwa na uelewa mdogo wa wanawake wa kijiji cha ugala,
juu ya madhara ya kiafya wanayoweza kupata.

BBC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *