Wanawake wa mkoa wa shinyanga wampongeza rais samia kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wanawake  Mkoa wa Shinyanga wameipongeza serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, maji na
miundombinu ya barabara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.

Wametoa
pongezi hizo leo Alhamis Oktoba 12,2023 kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa
Shinyanga ambalo limeratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
Mndeme kwa lengo la kumshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili
wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na kuchochea uchumi mkoani humo.

Kongamano
hilo limefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Savannah shule ya kimataifa na
kuhudhuriwa na wanawake mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa
Shinyanga ,wakiwemo wajasiliamali,wanasiasa,wakulima,watumishi wa serikali
makampuni,mashirika na taasisi binafsi.

 Katika taarifa 
yake aliyoitoa leo kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema  serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan imeendelea kuwekeza kwenye  sekta
zote hivyo kuchochea Maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika upatikanaji wa
huduma bora za kijamii

RC
Mndeme amesema serikali imeendelea kuboresha huduma za kijamii katika sekta
mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya,Maji, kilimo,viwanda na uwekezaji pamoja na
Miundombinu.

Amesema
Mkoa wa Shinyanga umepokea fedha takribani shilingi tirioni moja kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo
sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Ameeleza
kuwa ilani ya chama cha mapinduzi 2020/2025 imeendelea kutekelezwa kwa uwazi
,umahili na mafanikio ikiwemo makusanyo ya maduhuri na mapato ya serikali.

“Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga
tumeamua kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa sababu Shinyanga ya sasa siyo
Shinyanga ya zamani maendeleo makubwa tunayashuhudia ya kiuchumi naya kijamii
sisi wanashinyanga tunasema kila kijiji kimefikiwa kazi inaendelea kwa
vitendo”.

“Baadhi ya mafanikio ambayo
tumeyapata wanashinyanga na tunaendelea kuyapata kupitia uongozi thabiti wa
Dkt. Samia Suluhu Hassan makusanyo ya maduhuri na mapato ya serikali,
ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga umeongezeka kutoka
shilingi Bilioni 22 na Milioni 349 na laki nane na sita kwa Mwaka 2021/2022 na
sasa tumefikia makusanyo ya shilingi Bilioni 31 na milioni 263 na 41 elfu kwa
Mwaka 2022/2023 kupitia uongozi thabiti wa Mhe. Rais Samia makusanyo ya Halm
ashauri yameongezeka kwa asilimia 41”.

“Ongezeko hili linamalisha kuwa upelekeaji
na uboreshaji wa huduma kwa wananchi umeongezeka kwa asilimia 41 zikiwemo
ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya, zahanati, madarasa, matundu ya vyoo,
mabweni, masoko, nyumba za watumishi, usafi wa mazingira, uboreshaji wa bustani
za mji na kadharika”.amesema RC Mndeme

Amebainisha
kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 386 kwa shirika la usambazaji umeme  TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya mradi
wa kusambaza umeme vijijini ikiwa ni kwa awamu ya tatu mzunguko wa pili kwa
vijiji 240 kwa shilingi bilioni 60.8 kwa wilaya zote tatu

Aidha
katika Kongamano hilo mada ya kulinda maadili kwa jamii hasa watoto ni kati ya
mada zilizowasilishwa  kwa washiriki wa
kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.

Kupitia
kongamano hilo wanawake pia wamekumbushwa kuchangamkia fursa zote
zinazojitokeza mbele yao ikiwemo
  mikopo
inayotolewa na Halmashauri,taasisisi za kifedha ili waweze kujikomboa
  kiuchumi.

Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye kongamano la
wanawake wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye kongamano la
wanawake wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.

Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye kongamano la wanawake
wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akitoa salamu
za chama kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la
kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo.