Wapiga debe waifunga timu ya mnara wa voda 2-1 ligi ya dr. samia cup shinyanga

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Timu ya Wapiga debe imeibuka na ushindi wa
magoli mawili kwa moja katika mchuano wao na timu ya Mnara wa voda kwenye ligi
maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA.

Mchezo huo umefanyika katika uwanja wa
SHYCOM, na kwamba Mashindano hayo yameandaliwa na jumuiya ya vijana wa chama
cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa udhamini wa Taasisi ya Bega
kwa Bega.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga
mjini Jonathan Madete amewataja wafungaji katika mchezo huo.

“Wafungaji
katika timu ya Wapiga debe ni Ramadhan Mbaga na Gerlad Devid lakini goli la
timu ya Mnara wa voda limefungwa na Reonard John dakika za mwishoni”.
amesema
Mwenyekiti Madete

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha
mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira
wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Seleman Magubika ameendelea
kuwapongeza waandaaji wa mashindano hayo, UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini
kupitia udhamini wa Taasisi ya Bega kwa Bega.

 

 Awali wachezaji wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo wao leo Jumatano Agosti 30,2023.