Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Sara Maongezi
akifungua kongamano la kitaifa la wafiziotherapia nchini.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (Kulia)
akizungumza katika kongamano la wafiziotherapia linalofanyika katika
Hospitali ya Mloganzila, kushoto ni Dkt. Sara Maongezi.

Rais wa Chama cha Kitaaluma cha
Wafiziotherapia Tanzania (APTA), Bi. Remla Shirima akisoma risala wakati
wa Kongamano la Wafiziotherapia linalolenga kuangalia maendeleo ya
taaluma hiyo nchini.

Wataalam wa Fiziotherapia wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizotolewa katika mkutano huo.
Dkt. Sara Maongezi na Dkt.
Julieth Magandi wakiwa katika picha ya pamoja na wafiziotherapia mara
baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa mwaka wa wataalam hao.

Wataalam wa Fiziotherapia
wamekutana katika kongamano la kitaifa la taaluma ya tiba kwa vitendo
lengo likiwa ni kuangalia maendeleo ya taaluma hiyo nchini.

Akizungumza wakati wa kufungua
mkutano huo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Sara Maongezi amesema kuwa Wizara ya Afya
inazitambua kisheria huduma zinazotolewa na wafiziotherapia nchini.

“Huduma ya tiba kwa vitendo na
wanataalauma wake wanatambuliwa rasmi na sheria ya kusimamia huduma na
watoa huduma wa taaluma katika sheria mpya ya madaktari, madakari wa
meno na huduma shirikishi ya 2017 (Medical, Dental and Allied Health
Professionals Act 2017),” Amesema Dkt. Maongezi.

Awali akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kaimu Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi
ametaja kuwa hospitali ina jumla ya vitanda 608 ambapo kwa siku
inahudumia wagonjwa wa nje 400 hadi 450, na wagonjwa wa ndani takribani
300 ikiwa ni pamoja na kufanya upasuaji kwa wagonjwa 200 hadi 300 kwa
mwezi.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha
Kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania, Bi. Remla Shirima ametaja moja
kati ya changamoto ambayo taaluma hiyo inapata ni kukosekana kwa vyuo
vinavyotoa shahada ya taaluma ya tiba kwa njia ya vitendo ambapo hadi
sasa vyuo vingi hapa nchini vinatoa elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada
tu.

“Tunaiomba Serikali kupitia Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania ianzishe vyuo vinavyotoa shahada ya tiba kwa njia
ya vitendo kutokana na idadi ya wataalam hawa kuwa wachache, ambapo
hadi sasa wapo takribani wataalam 400 nchini na kati ya hao 182 tu ndio
wanaofanyakazi kwenye taasisi za Serikali kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa mapema mwaka huu,” Amesema Shirima.

Kongamano limejumuisha washiriki
wanaotoka sehemu mbalimbali nchini ikiwamo wataalam kutoka MNH, Chuo cha
Fiziotherapia KCMC, Benki ya NMB, Wawakilishi kutoka Chuo cha
Fiziotherapia SOMT nchini Netherlands, Bodi ya Usajili wa Hospitali
Binafsi za Afya nchini (PHAB), Taasisi za Hospitali Binafsi (APHTA),
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Wawakilishi wa vyama mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi, Kamati tendaji ya Chama cha Kitaaluma cha
Wafiziotherapia Tanzania (APTA), Dawati la utengamao-Wizara ya Afya na
Baraza la Habari Tanzania (MCT).