Watanzania wategemee mageuzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji

 

Aliyesimama Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya, akikagua
mtambo aina ya Wheel loader wenye kazi ya kuchota kifusi, alipotembelea
katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukagua mitambo hiyo

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akitoa
maelekezo ya kutumika kwa mtambo mpya unaotumika katika ujenzi wa
miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili isipate kutu wakati wa mvua.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiendelea
na ukaguzi wa Mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa
Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma leo.

Katibu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema,
watanzania wategemee mageuzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji, kwani serikali
ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekata
hiyo.

Bw. Kusaya ameyasema
hayo jijini Dodoma alipokuwa na ziara ya kikazi katika ofisi za Tume ya Taifa yaUmwagiliaji,
ambapo amesema Serikali ina mpango wa kuboresha mundombinu yote chakavu katika sekta
ya umwagiliaji na kufufua skimu za zamani na kuongeza skimu mpya.

Alisema pia
ikiwemo kuongeza vyanzo vipya vya maji katika maana ya kujenga mabwawa na kutumia
vyanzo asili vilivyopo kama mito, mabwawa 
ya asili na maziwa hivyo mkulima atanufaika na kilimo cha umwagiliaji katika
mazao ya biashara na chakula.

Sambamba na hilo,
amesema Serikali pia imeona umuhimu wakuongeza wataalamu wa sekta hiyo katika ngazi
za wilaya na itafikia ngaz iya kata na kijiji ili kuweza kumfikia mkulima kwani
kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo cha uhakika na mkombozi kwa mkulima.

“wakulima watapata
huduma za uhakika zaidi na kunufaika na kilimo cha umwagiliaji” Alilisita.

Awali,
alipokuwa akizungumza na menejimenti yaTume ta ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw.
Kusaya amewataka watumishiwa Tumeya Taifa ya umwagiliaji kufanya kazi kwa ushirikiano,na
uhakika ili kuweza kufikia malengo ya mageuzi makubwa yenye tija katika sekta ya
umwagiliaji.

Na baada ya hapo
katibu Kusaya alikagua mitambo iliyopo katika ofisi za Tume hiyo inayotumika kujengea
na kuboresha miuondombinu ya umwagiliaji.

kulia Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akikagua gari
iliyotoka site aina ya fuso lenye kufanya kazi ya kubeba kokoto,mchanga
na mawe katika kazi za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, gari hilo
lina uwezo wa kubeba tani kumi na tano, kushoto ni kaimu mkurugenzi Mkuu
wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali.