Watatu wauawa kwa tuhuma za ujambazi tarime…mmoja adakwa akiwa na damu kwenye gariKamanda wa Polisi Tarime/Rorya Henry
Mwaibambe akionyesha silaha iliyokamatwa na Polisi wakati wakikabiliana
na watuhumiwa wa ujambazi
Na Dinna Maningo – Malunde 1 blog Tarime.
Watu watatu wanaotuhumiwa kwa ujambazi
wameuawa wakati wakijaribu kuwashambulia askari polisi kwa risasi katika
kijiji cha Obwere -Shirati wilayani Rorya mkoani Mara. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime
/Rorya Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea Novemba 7 ,2019
majira ya saa nne usiku baada ya watuhumiwa hao walipovamia nyumbani kwa
David Ogutu maarufu (Baba Ouma)kwa lengo la kutaka kuiba mali.


Alisema k katika mashambulizi hayo
polisi walifanikiwa kuwanyang’anya silaha mbili aina ya AK 47 ikiwa na
risasi tano na nyingine ya Kienyeji ambayo maganda yake hayajapatikana.

“Walivamia majambazi watano ila kwa
bahati nzuri Ogutu alipiga simu Polisi na polisi waliwahi eneo la tukio
na ndipo majambazi wakaanza kuwarushia polisi risasi, Polisi nao
wakajihami na hivyo kufanikiwa kuwajeruhi watatu ambao  walipoteza
maisha na wawili wakakimbia,tunawatafuta”,alisema.
“Mmoja aitwae Kisante Chacha (19)yeye
alikimbia akiwa amejeruhiwa na kutoka damu tulimkamata akiwa kapanda
gari zinazokwenda Sirari maana tulikuwa tulishawajulisha wananchi popote
watakapoona mtu ana majeraha ya damu watoe taarifa na wakatupa
ushirikiano,nguo zilikuwa na damu kutokana na majeraha ya
risasi”,alisema Mwaibambe.

Kamanda huyo alieleza kuwa mtuhumiwa
huyo alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi huku John Marwa ambaye nae
alikuwa amejeruhiwa kwa risasi alikutwa  kwenye nyumba ambayo haijaisha
akiwa amekufa.
“Mwaka juzi kama tulivyosikia kwenye
vyombo vya habari kuwa Mwanamke kapambana na Jambazi alikuwa ni huyu
Kisante, tulimkamata akafikishwa mahakamani kwa kuwa umri wake ulikuwa
chini ya miaka 18 alifungwa kifungo cha nje na baadae akaendelea na
vitendo vyake viovu.
Mwaibambe amewashukuru wananchi wa Rorya
na Tarime kwa ushirikiano wao ambao ulifanikisha kuwakamata baadhi ya
waharifu huku akiwataka vijana kutafuta mali kwa njia halali.