Watoto 1000 wanaozaliwa nchini, watatu huzaliwa na ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga wakati wa maadhimisho ya siku  ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga 

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Jonathan Budemu akizungumza wakati wa maadhimisho hayo 

 Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na
Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo kushoto ni 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga 

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimkabidhi cheti Mfanyakazi wa Benki ya NMB Jeniffer Mtey kwa ajili ya udhamini wa maadhimisho hayo 

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto
akimpongeza mtoto mwenye ulemavu wa kichwa kikubwa Joaly Salehe  ambaye
aliimba wimbo wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella akifuatiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda
Mtondoo

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari

NA MWANDISHI WETU,TANGA

 WATOTO 1000
wanaozaliwa kila siku nchini watatu wanazaliwa wakiwa na matatizo ya ulemavu wa
kichwa kikubwa na mgongo wazi idadi ambayo imeelezwa kwa mwaka inafikia watoto
4800.
Takwimu
hizo zilitolewa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo
wazi duniani.
Maadhimisho
hayo yalifanyika Kitaifa kwenye viwanja wa Tangamano mjini Tanga ambapo alisema
kwamba serikali imekuwa ikiweka juhudi kubwa kuweza kuhakikisha inatokomeza
suala hilo.
Alisema
kwamba wakati umefika jamii kuacha kuwa na mila potofu kwa watoto wenye vichwa
vikubwa na mgongo wazi na dhana hiyo ianze kwa wazazi, walezi na familia
inayowazunguka.
“Kwani
imani potufu ndio zimepelekea wazazi na walezi wa watoto hao kutumia fedha nyingi
kwa waganga wa kienyeji bila mafaanikio na kusababisha ongezeko la vifo vya
watoto wao”Alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy
aliitaka jamii kutambua kwamba mtoto akizaliwa na kichwa kikubwa sio
laana,mkosi wala balaa huku akiwataka kuachana na imani potufu kwani wameambiwa
na wataalamu chanzo cha watoto kuzaliwa hivyo ni kutokana na upungufu wa madini
ya foliki Acidi na virutubisho muhimu vinavyotokana na kwenye vyakula nyingi
vilivyopo hapa nchini,.
“Lakini pia
niwaase wakina mama wajawaziti kutumia vitamin hiyo kabla ya kupata ujazito huku
akitoa wito kwa wanawake wenye umri wa kuzaa miaka 15 hadi 49 kuzingatia ulaji
bora wa vyakula vyenye vitamin ya aina ya foliki acidi ikiwemo mbogamboga na
matunda”Alisema Waziri Ummy
Hata hivyo
alisisitiza umuhimu wa kila mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa wajawazito kwenda
kliniki mapema mara wanapogundua ni wajawazito ili waweze kupatiwa huduma za
afya ikiwemo vidonge vyenye vitamini ya foliki acid.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella alisema kwamba tatizo hilo linazuilika na kumalizika kabisa kwenye jamii
kwa kutoa elimu namna ya kuepukana nalo.
Mkuu huyo
wa mkoa pia aliwataka viongozi wa dini kushirkiana na wadau katika kutoa elimu
kwa jamii kwani tatizo hilo linaweza kuwa historia kama elimu sahihi inaweza
kupatikana kwa wakati.
Naye kwa
upande wake Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na
Watu Wenye ulemavu Joyce Maongezi alisema kwamba jamii inapaswa kutambua mapema
watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.
Alisema
kwamba ofisi yao itaendelea kutoa vifaa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo
kuielimisha jamii pamoja na kuzindua mfuko wa Taifa wa watu wenye ulemavu ambao
utaweza kuwasaidia.

“Lakini pia
Halmashauri zitekeleze agizo la Serikali za kutaka watenge asimilia 2 ya mapato
yake kwa ajili ya watu wenye ulemavu “Alisema