Watumishi wa umma watakiwa kuendana na wakati kiutendaji

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.
Aggrey Mwanri akielezea historia fupi ya Mkoa wa Tabora kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe.
Anders Sjoberg walipomtembelea ofisini kwake jana kabla ya kutembelea
Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kwa lengo la kuona
maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya
Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa
Wilaya ya Tabora Mjini, Mhe. Kitwala Komanya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri
na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kuingia Chuo
cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo
ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na
Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakiungana na
wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora
na wageni wengine kucheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na bendi ya
Msange JKT wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma
Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho
kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka
1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Alex Massengo akiwaonyesha
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey
Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg matukio
mbalimbali katika picha yakiwemo yanayohusu ushirikiano wa Serikali ya
Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya
Tabora wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi
la Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho.Mkuu wa Idara ya Uhazili,  Chuo
cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Given Simkwai akiwaonyesha
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey
Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg umuhimu
wa  matumizi ya hati  mkato wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha
Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya
chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na
Sweden mwaka 1970.Na Mary Mwakapenda, Tabora 
Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kubadilika kiutendaji ili kuendana na  kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayotokea hivi sasa duniani kwa lengo la kuliletea taifa letu maendeleo.


Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg iliyolenga kuangalia maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya
Tabora kilichojengwa mwaka 1970 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania
na Sweden.


Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema hivi sasa kila kitu kinabadilika duniani
ikiwemo uchumi, maisha na teknolojia, hivyo watumishi wa umma hawana
budi kubadilika kulingana na wakati uliopo, kwa mantiki hiyo ni lazima wawe wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hatimaye taifa liweze kunufaika na mchango wao.


“Kama katika sekta binafsi wanafanya kazi ipasavyo kwanini katika Sekta ya Umma tushindwe? ikizingatiwa kuwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wanahitaji huduma kutoka serikalini na waliopewa dhamana ya kuwahudumia ni sisi,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihoji na kuongeza kuwa, ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi makini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inasisitiza na kuiishi kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ili watumishi wa umma wawe na tija kwa taifa.


Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewasisitiza watumishi na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza wajibu wake ipasavyo ili kutimiza malengo waliyojiwekea.


“Ukiwa mwanafunzi soma kwa bidii na mtumishi fanya kazi kwa bidii ili kutimiza ndoto yako kwani Serikali inataka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kiendelee kutoa mchango katika maendeleo ya taifa na kuwa mfano bora wa kuigwa na vyuo vingine” Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza.


Akitoa salamu za Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri amemshukuru Naibu Waziri na Balozi Sjoberg kwa ujio wao kwani unaendelea kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden ambao ulianza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza mpaka sasa.


Mhe. Mwanri amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kutumia vema ujuzi watakaoupata kwa manufaa yao na maslahi ya taifa na kuongeza kuwa chuo hicho kina historia ya kutoa viongozi bora huku akitoa mfano wa baadhi ya viongozi waliosoma hapo na kupata mafanikio makubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu na Mke
wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Hayati Robert Mugabe, Mama Grace
Mugabe.


Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaasa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kutekeleza wajibu wao ipasavyo, na hakusita kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kukiendeleza chuo hicho.


Ziara hiyo ilitoa fursa kwa viongozi hao kutembelea maktaba ya kumbukumbu, maktaba, chumba cha Kompyuta, darasa la kupiga chapa, mabweni ya wanafunzi na jengo jipya la utawala linalojengwa kwa fedha za ndani ambalo limekamilika kwa asilimia 94 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.