Waumini wakumbushwa kuuishi upendo kwa matendo parokia ya lubaga shinyanga

Waumini wa kanisa katoliki parokia ya Lubaga Mjini
Shinyanga wamekumbushwa wajibu wa kuuishi upendo wa Mungu kwa matendo ya
kweli,ikiwa ni pamoja na kusaidia wenye uhitaji.

Mafundiyo hayo yametolewa na shemasi James Mrema wa
parokia ya Lubaga wakati akihubiri katika adhimisho la misa takatifu ya
jumapili iliyokwenda sanjari  na kuombea
marehemu waliofariki Dunia kwenye ajali ya Meli ya MV Bukoba mnamo  Mei 21, 1996 Mkoani Mwanza

Amesema ni wajibu wa kila Mkristu kuuishi upendo wa
Mungu kwa kuwasaidia kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaombea watu
wengine wakimemo wagonjwa,na wale waliotangulia mbele za Mungu ambao wanahitaji
huruma ya Mungu

Shemasi James amesisitiza kuhusu wajibu wa kumtumikia
Mungu katika Imani ya kweli,kushiriki ibada, na matendo ya huruma.

Waumini wa kanisa katoliki parokia ya Lubaga Mjini
Shinyanga wameungana na watanzania wengine Nchini kuwakumbuka ndugu,jamaa na
marafiki walipoteza maisha kutokana na ajali ya Meli ya Mv Bukoba mnamo Mei 21,
Mwaka 1996

Katika serikali iliwakilishwa na Neema Mkandala kwa
niamba ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ambaye katika salamu zake amewakumbusha
ndugu na jamaa waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba  pamoja na mambo mengine amesema watanzania
wanapaswa kuishi maisha yanayompendeza Mungu, ikiwa ni pamoja na kupinga
ukatili unaoendelea.

“Katika
kuendelea kuwaenzi wapendwa wetu tukumbuke kufanya matendo mema yakumpendeza
Mungu serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kukemea vitendo viovu vya
mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu na kukemea ukatili wa kijinsia, katika
kuwaenzi ndugu zetu niwaombe waumini wote tuwe msitari wa mbele katika kutoa
taarifa kuhusiana na ukatili unaofanyika katika jamii zetu kwenye vyombo husika
na tufanye matendo mema kwa kuwa na maadili yakumpendeza mwenyezi Mungu”.
Amesema
Neema Mkandala