Wadau wa
mafuta ya kula Nyanda za Juu Kusini wakifuatilia kwa karibu mafunzo
yaliyotolewa na TBS kwa kushirikiana na BRELA, SIDO na Wakala wa Vipimo.
Wazalishaji
wa mafuta ya kula wametakiwa kufuata kanuni bora za kilimo, usindikaji
na zile za afya ili kuongeza uzalishaji nanubora wa bidhaa hiyo nchini.
Wito
huo ulitolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa mafunzo
kwa wasindikaji, wauzaji, wasambazaji na wenye maduka yanayouza mafuta
wapatao 972 yaliyofanyika katika mikoa minne ya nyanda za juu kusini
kuanzia February 19 hadi 29 mwaka huu.
Mafunzo
hayo yalihusisha wadau hao kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na
Mbeya ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kupitia Wizara ya
Viwanda na Biashara kutaka wazalishaji wa mafuta nchini kusaidiwa ili
waweze kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyi.
Kwa
sasa mafuta ya kula yanayozalishwa nchini ni tani 200, 000 kwa mwaka,
wakati mahitaji halisi ni kati ya 400,000 hadi 600,000.
Mafunzo
hayo yalihudhuriwa na BRELA, SIDO na Wakala wa Vipimo (WMA), ambapo
kila mmoja alieleza wadau hao nafasi yake katika kufanikisha uzalishaji
na ukuzaji biashara ya mafuta.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Udhibiti Ubora wa Bidhaa TBS,
Baraka Mbajije, aliwataka wazalishaji wa mafuta kufuata kanuni bora za
kilimo, usindikaji pamoja na za afya.
Mbajije
alisema kanuni bora za kilimo zinahusiha mbegu bora, kuvuna kwa wakati
na mazao yanayovunwa kwa ajili ya uzalishaji mafuta yanatakiwa yawe
yamekomaa.
Kwa
upande wa kanuni bora za usindikaji kwa mujibu wa Mbajije ni pamoja na
kuzingatia usafi hasa kwenye mazingira ya viwandani.Alisema mazingira ya
uzalishaji viwandani yanatakiwa kuwa safi pamoja na mashine
zinazotumika.
Akizungumzia
kanuni bora za afya, Mbajije alisema wazalishaji wanatakiwa kuhakikisha
vifaa vya kuhifadhi mafuta ni safi ikiwa ni pamoja na madumu
yanayotumika kuhifashi mafuta hayo yawe yamesafishwa vizuri.
”
Madumu wanayoweka mafuta wahakikishe wameyasafisha vizuri na waweke lebo
zinazoeleza bidhaa hizo ni za aina gani,” alisema na kuongeza kwamba
haikubaliki kwenye vifungashio ambavyo wazalishaji wanaweka mafuta iwe
lebo inayohusu bidhaa nyingine.
Aidha,
alisema mafuta ya kula hayatakiwi kuwekwa juani, kwani yanapokuwa juani
kuna kemikali zinazozalishwa na zinaweza kusababisha magonjwa ikiweno
kansa.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Abel
Mwakasonda, alitoa mwito kwa wadau hao kusajili TBS majengi ya bidhaa za
vyakula na vipodozi.
Alisema kwa kufanya hivyo Shirika hilo litaweza kuwafikia kwa urahisi.
” Tunatoa mwito kwa wadau kufika TBS, wasiogope kama kuna makosa tutawasaidia kuyarekebisha,” alisema Mwakasonda.
Alisema
ni muhimu kwa wafanyabishara kusajili bidhaa na majengo ya vyakula na
vipodozi kwa mujibu wa sheria ambayo imetokana na mabadiliko ya Sheria
ya fedha ya mwaka 2019.
Sheria
hiyo ilirudisha majukumu ya usimamizi wa usalama na ubora wa vyakula na
vipodozi kwa TBS kutoka kwa iliyokua Mamlaka ya Dawa na Chakula
Tanzania (TFDA).
Alisema usajili wa bidhaa majengo ya vyakula na vipodozi ni takwa la kisheria ili kuwawezesha kufanya biashara zao urahisi.
Usajili
majengi ya biashara unawapa wafanyabiashara uhakika wa kutunza bidhaa
na wanasajili jengo kulingana na bidhaa zinazoenda kuhifadhiwa humo.
Kwa
upande wa usajili wa bidhaa, eneo linalohusika ni bidhaa za chakula na
vipodozi.Usajili wa vipodozi vilivyopigwa marufuku kwenye soko la
Tanzania haviingizwi nchini kutokana na kuwa na viambata sumu.
Mafunzo
hayo kwa wazalishaji wa mafuta ni mwendelezo wa mafunzo yaliyokwisha
kutolewa katika mikoa Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma.