Waziri aweso awasha moto morogoro amtumbua kigogo wa moruwasa

 

 

Na Mwandishi,Morogoro

  

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewasimamisha
kazi vigogo wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (Morowasa) ili
kupisha uchunguzi wa wa tuhuma ambazo zinawakabili huku akiagiza watumishi
wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

 

Vigogo waliosimamishwa kazi kupisha
uchunguzi ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro
(MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba,Afisa Maji wa Bonde la Wami Ruvu Bwana
Simon Ngonyani huku akiagiza watumishi wengine waliokuwa vinara wa kueneza
chuki na kuleta taharuki badala ya kufanya kazi nao wachukuliwe hatua za
kinidhamu.

 

Waziri Aweso aliyasema hayo wakati
akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo alisema kuwa Mkurugenzi
wa Moruwasa pamoja na tuhuma nyingine za kiutumishi lakini alisaini mkataba wa
fedha nyingi na wakandarasi bila kushirikisha Wizara na hata bila uwepo wa
Katibu Mkuu kinyume na taratibu.

 

Huku Afisa  wa Bonde
akisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi.