Waziri hasunga amtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kanda ya sumbawanga

Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati  akizungumza
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA)
Ndg Milton Lupa na Meneja wa 
Wakala
wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah
Nyangasa mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga
mkoani Rukwa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya KIlimo)
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala
na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi
huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati  akizungumza
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA)
Ndg Milton Lupa (Kushoto) na Meneja wa 
Wakala
wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah
Nyangasa  (Kulia) mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya
Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala
na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi
huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg
Milton Lupa na Meneja wa 
Wakala
wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah
Nyangasa sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa NFRA mara baada ya
kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
 
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Katavi

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maghala na vihenge vya
kisasa kanda ya Sumbawanga kuongeza kasi ili kukamilisha haraka mradi
huo kwa mujibu wa makubaliano.

Alisema kuwa kampuni iliyoteuliwa
baada ya kushinda zabuni kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo ni UNIA ARAJ
REALICZJE ya nchini Poland ambayo ilimteua mkandarasi msaidizi mzawa
anayejulikana kwa jina la ELERAI CONSTRUTION CO. LTD wa Arusha, hivyo
napaswa kuongeza kasi ya ujenzi kutokana na kasi iliyopo kwa sasa
kutoridhisha.

Waziri Hasunga ameyasema hayo juzi
tarehe 10 Octoba 2019 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo
kwenye Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi utakaowanufaisha wakulima wa
mazao ya nafaka kwani serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB)
itakuwa na uwezo wa kununua mazao mengi kwa wakulima na kuyahifadhi kwa
muda mrefu.

Alisema kuwa kampuni hiyo inayojenga
vihenge vya kisasa na miundombinu mingine ikiwemo maghala katika eneo
la Kanondo Manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa na Mpanda Mkoani Katavi
bado haijamfurahisha kutokana na kasi ndogo ya ujenzi wa mradi.

Mhe Hasunga amesema kuwa serikali
imekusudia kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka nchini ili kuwanufaisha
wakulima punde wanapovuna mazao yao hususani nafaka kwani kufanya hivyo
wakulima wataongeza uzalishaji na tija kwenye mazao na kuliongezea Taifa
pato kubwa.

Alisema kuwa vihenge hivyo vitakuwa
na uwezo wa kuhifadhi jumla ya Tani 20,000 za nafaka huku ujenzi wa
miundombinu mingine ukiendelea kama jingo la Ofisi ya utawala, Ghala la
kawaida la ujazo wa Tani 5000 za nafaka, na Mzani mkubwa wa daraja
(Electronic weighbridge).

Mradi huo utakuwa na gharama ya Dola
za kimarekani 6,019,399 ambazo ni takribani shilingi za Kitanzania
Bilioni 14 kwa mradi wa eneo la Kanondo Sumbawanga na vilevile Dola za
Kimarekani 6,180,857 sawa na fedha za kitanzania Shilingi Bilioni 14.2

Mhe Hasunga ametilia nyundo kuwa
serikali haitaongeza muda kwa mkandarasi endapo atashindwa kukamilisha
mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Muda wa mradi kuanza hadi kukamilika
ni jumla ya miezi 18 (Mwaka mmoja na nusu), Kwa upande wa Mpanda mkoani
Rukwa mradi umeanza tarehe 14 Januari 2019 na umepangwa kukamilika
tarehe 14 Julai 2020 wakati upande wa Kanondo mkoani Katavi mradi huo
umeanza tarehe 8 Septemba 2019 na unatarajiwa kukamilika tarehe 8 Machi
2021.

Punde mradi huu utakapokamilika mkoa
wa Rukwa utakuwa na Maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka za Tani 58,500 wakati mkoa wa
Katavi utakuwa na uwezo wa kuhifadhi Tani 28,000 ikihusisha pia maghala
ya zamani.