ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya
wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua
miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo)
ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya
wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua
miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.
ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya
wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua
miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kubadili
matumizi ya gharama za uchimbaji wa visima kutoka Tsh Milioni 160 mpaka
kuchimba kwa Tsh Milioni 20.
Waziri Hasunga
ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2019 wakati akizungumza na wananchi
mara baada ya kutembelea skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Amesema kuwa
gharama za uchimbaji wa kisima kimoja kwa ajili ya umwagiliaji haipaswi
kuzidi shilingi Milioni 20 kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu
na kushindwa kuakisi kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Katika ziara hiyo
Waziri Hasunga ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuchimba visima
vitatu katika eneo hilo kwa kiasi cha shilingi milioni 60 ikiwa ni
shilingi milioni 20 kwa kila kisima kimoja.
Amesema kuwa
umefika wakati wa wakulima kuachana na kilimo cha kutegemea mvua za
msimu badala yake kuhakikisha kuwa wanalima kilimo bora cha umwagiliaji.
Kadhalika
amekumbushia agizo lake alilolitoa hivi karibuni la kila mkoa kuwa na
Afisa umwagiliaji wa mkoa huku wilaya zote zenye skimu za umwagiliaji
kuwa na afisa umwagiliaji wa wilaya.
Waziri Hasunga
amesema kuwa mkakati huo madhubuti wa serikali kuhakikisha kunakuwa na
skimu nyingi za umwagiliaji utaimarisha sekta ya kilimo jambo
litakaloongeza kipato cha mtu mmoja mmoja sambamba na Taifa kwa ujumla
wake.
Kuhusu mkakati wa
serikali kuwa na kiasi kikubwa cha umwagiliaji, ameiagiza Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka miwili kuongeza eneo la
umwagiliaji ili kufikia hekta milioni moja huku kakiongeza kuwa hadi
kufikia mwaka 2025 eneo la umwagiliaji liwe limefikia Hekta milioni
tano.
Kwa upande wake
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda amewapongeza wakulima wa skimu
hiyo kwa kuimarisha sekta ya kilimo huku akisisitiza kuwa serikali
inapaswa kuongeza mkakati madhubuti wa kuimarisha masoko ya mazao ya
wakulima.
Kwa upande wake
Mkuu wa idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri Wilaya ya
Mtwara Ndg Joseph Tesha akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri wa Kilimo
amesema kuwa skimu hiyo ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere
inayohudumia vijiji vya Lilido na Chemchem ina jumla ya eneo la Hekta
920 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku eneo lililoendelezwa
likiwa ni jumla ya Hekta 310 pekee.
Waziri Hasunga
yupo mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo awali alitembelea
mkoa wa Pwani na Lindi kwa ajili ya kukagua hali ya uuzaji wa korosho
msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa
korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na kukagua
skimu za umwagiliaji.