Waziri kalemani akagua tena utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa julius nyerere mw 2115

WAZIRI
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua
maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius
Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa
utekelezaji wake.




 Dkt.
Kalemani ameridhishwa na hatua mbalimbali ambazo mradi huo
unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa mikoa ya Pwani na
Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi. 



Aidha,
alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote
wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine
wa mradi wawe wamehamia. 



“Wafanyakazi
wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na
haraka”, alisema Dkt. Kalemani. Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu
utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi
wasaidizi. 



Mkataba
wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu
Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi
Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha
miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi
wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022


 Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa
ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115
(JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati
alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi  huo.
 Dkt.
Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO
Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo leo Januari
12, 2019.