Waziri kalemani asisitiza matumizi ya gesi ili kupunguza uharibifu mazingira

Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani
,akizungumza leo na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini katika
mkutano wa majadiliano ya Wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa
Madini Stanislaus Nyongo,akizungumza leo na washiriki kutoka Taasisi
mbalimbali nchini katika mkutano wa majadiliano ya Wiki ya Azaki
inayoendelea jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini waliojitokeza katika mkutano wa wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma.
………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
 Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani amesema
kuwa serikali imeendelea kusisitiza katika matumizi ya gesi kwa wananchi
ili kupunguza uharibifu wa mazingira ndani ya nchi.
Hayo ameyasema leo
alipokuwa akizungumza na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini
katika mkutano wa majadiliano ya Wiki ya Azaki inayoendelea jijini
Dodoma.
 
Dk Kalemani amesema kuwa wananchi kwa sasa
wameanza kujenga  mazoea ya kutumia gesi lengo ni kupunguza ukataji wa
miti hovyo ambayo inachangia kuharibu mazingira.
Amesema sekta ya uziduaji ni  muhimu sana ambayo
inapaswa kutunza ili iweze kuleta manufaa katika nchini jambo ambalo
linahitaji kuangaliwa.kwa.kiasi.kikubwa.
Waziri Kalemani amesema kuwa kwa sasa tunahitaji kutumia gesi kwa kuhakikisha rasimali hizo zinatumika ipasavyo.
Dkt.Kalemani amesema
kuwa Tanzania inarasimali kubwa ya gesi lakini bado hatujagundua
Mafuta,ila jitihada za serikali kutafuta zinaendelea.
Amesema kuwa  kwa upande wa gesi
toka trion mbili trion 57.5 jambo linalopaswa kuipongeza serikali ya
awamu ya tano,hivyo Trion 57.5 zinapaswa kupongezwa kutokana na ongezeko
hilo.
Akizungumzia kuhusiana na suala Mafuta amesema kuwa serikali inaendelea na jitihada za utafutaji Mafuta.
Aidha waziri Kalemani amewataka
AZAKI kutoa taarifa sahihi na zitoke kwa wakati ili wananchi waweze
kujua nini kinaendelea ikiwemo kupata takwimu sahihi.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa
Madini Stanislaus Nyongo,amesema kuwa Serikali imejipanga kuanza
kusafisha dhahabu hapa nchini ili kuongeza thamani yake hali
iatayosaidia kuongeza pato la taifa na kuhifadhi fedha Benki kuu kwa
ajili ya matumizi mbalimbali ya baadae.
Aidha amesema kuwa watajenga 
kituo cha kuchakata dhahabu jijini Dodoma na mkoani Geita vyote
vitatumika kwa ajili ya kusafisha dhahabu lengo likiwa ni kuongeza
thamani ikiwemo pato la taifa litokanalo na dhahabu.
Mhe.Nyongo amesema kuwa dhahabu
inayopatikana hivi sasa ni asilimia 80 wanahitaji isafishwe hapa nchini
na.kufikia asilimia 99.9 ili BOT iweze kupata fedha kutokana na dhahabu
hiyo.