Waziri lugola amtaka rpc morogoro arudi kilimanjaro haraka

WAZIRI 
wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amemwagiza Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro, Hamis Issa kurudi Mkoani Kilimanjaro na kuhakikisha
Mwananchi Hemed Mbaga anatolewa mahabusu kutokana na kubambikiziwa kesi.

Pia
amemwagiza OCD wa Dodoma Mjini, Joas Steven kumpa orodha ya askari
ambao wamekuwa wakiwabakizia kesi madereva  bodaboda na bajaji wa Dodoma
ili aanze kushughuka nao.

Lugola
ametoa agizo hilo jana Septemba 22,2019 katika bonanza lilofanyika
uwanja wa shule ya msingi Chang’ombe jijini Dodoma baada ya  kukutana na
waendesha bodaboda na bajaji ili kusikiliza kero zao.

Waziri
Lugola amesema Julai  18,2019 Polisi mkoani Kilimanjaro walimkamata
Mbaga wakati alipokwenda kuangalia mkusanyiko wa watu kufuatia bodaboda
wawili kutelekeza fulushi la bangi.

“Maofisa
wa halmashauri walikuwa wanapita hapo kuelekea kwenye makusanyo lakini
walikuwa wa kwanza kufika na ndipo Mbaga akaja akitokea nyumbani lakini
cha ajabu wakambambikiza kesi na kumweka mahabusu hadi leo,” amesema
Lugola.
 
Kwa
mujibu wa Waziri, taarifa zilimfikia na akaagiza mtuhumiwa atolewe
haraka mahabusu lakini cha ajabu hadi jana alikuwa hajatolewa huku RPC
akihamishiwa Morogoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *