Waziri lugola asema serikali itaendelea kufuata misingi ya kidemokrasia kwa kuzingatia na kulinda haki za binadamu

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola amesema kuwa serikali ya
Tanzania  imekuwa  ikijidhatiti katika kufuata Misingi ya Kidemokrasia
kwa kuzingatia na kulinda na kutetea haki za Binadamu.


Waziri
lugola ameyasema hayo Septemba 26,2019  Jijini Dodoma wakati akizindua
Ofisi ya kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC,ambapo amesema katika
kuyatekeleza hayo  kwa vitendo serikali ya  Tanzania ni miongoni mwa
nchi chache zenye katiba ambazo ndani mwake zimeonesha bayana masuala ya
haki za binadamu na Utawala Bora.

Hata
hivyo,waziri lugola amesema serikali imetoa fursa kwa Asasi za  kiraia
kuanzishwa na kufanya kazi ya kuwajengea wananchi uwezo juu ya masuala
mbalimbali ya kiraia ikiwemo sheria , haki za binadamu na uwajibikaji .

 Katika
hatua nyingine Waziri Lugola amesema ujio wa Kituo cha sheria na haki
za binadamu (LHRC) Jijini Dodoma ni fursa kwa wanachi wa Dodoma na mikoa
ya kanda ya kati kwa ujumla .

Akisoma
Hotuba mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu Bi Anna Henga amesema kituo hicho kimekuwa kikifanya
tafiti mbalimbali hususan masuala ya Haki za Binadamu.

Sanjari
na hayo Bi Henga amesema kuanzishwa kwa ofisi jijini Dodoma imetokana
na msukumo usio zuilika wala kukwepeka wa kudumisha mashirikiano hayo na
serikali pamoja na Bunge.

Uzinduzi
wa ofisi hiyo unalenga  kudumisha mahusiano ya kikazi baina ya taasisi
za kiserikali  kama vile Bunge na mahakama hasa ukizingatia  kuwa
taasisi zote za kiserikali zimeshahamia Jijini hapa kufuatia dhamira ya
dhati ya serikali  ya awamu ya tano ya kuifanya Dodoma kuwa makuu ya
Nchi .

Kituo
cha kisheria na haki za Binadamu ni Asasi ya kiraia  isilofungamana na
itikadi zozote za kisiasa hivyo imekuwa ikitetea watu wote bila kujali
itikadi zozote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *