Waziri lukuvi amfyatua mkurugenzi nhc kwa uzembe, akagua ujenzi wa mradi wa machinjio vingunguti

Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akitoa maagizo ya kumvua cheo Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki
Shirika la Nyumba (NHC) baada ya kugundua uzembe kazini kuhusu
upangishaji wa nyumba ya NHC iliyopo Muhimbili jijini Dar es salaam.
…………………………………………
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amemvua cheo  Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki Shirika la Nyumba
(NHC) baada ya kugundua uzembe kazini na kusababisha upotevu wa fedha za
serikali kutokana na moja ya nyumba iliyopo Muhimbili jijini Dar es
salaam kupangishwa kinyume cha uKAKA HUJAMBO POLE KWA USUMBUFU NAKUOMBA
UTUMIE HIZI CODES KWENYE ILE STORY YA NHC ZA AWALI ZINA MAKOSA KIDOGO
MKUU taratibu wa shirika hilo.
Akizungumza katika eneo la tukio
Waziri Lukuvi leo amemwagiza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk.Maulid
Banyani kumuondoa katika nafasi hiyo na kuangalia wote waliohusika au
kushiriki kwa upotevu wa fedha hizo kuchukuliwe hatua za kinidhamu.
Mtu mmoja ambaye hakutajwa jina
lake amewapangisha wafanyabiashara mbalimbali katika jengo hilo
wakimlipa kiasi cha shilingi laki moja 100,000 kila mmoja kwa mwezi 
huku yeye akililipa shirika la nyumba (NHC) kiasi cha shilingi elfu
ishirini na Nne 24,000 kwa mwezi.
Wapangaji hao wamepanga katika
jengo hilo kwa muda wa miaka 13 na wamekuwa wakimlipa mtu huyo kiasi
hicho kila mwezi jambo ambalo linalikosesha mapato shirika la nyumba pia
Mamlaka ya Mapato TRA haikusanyi kodi ya serikali kutokana na
udanganyifu huo uliofanyika kwa muda mrefu na kusababisha upotevu wa
fedha nyingi za serikali.
Waziri Lukuvu ameongeza kuwa kama
Mkurugenzi huyu wa Miliki katika shirika la nyumba (NHC) ameshindwa
kuchukua hatua kwa ubadhirifu uliopo kwenye nyumba ya hapa Muhimbili tu.
ataweza kugunda na kuchukua hatua katika majengo yaliyopo nchi nzima
maana yake ni fedha nyingi zinapotea kwa uzembe huu.
“Huyu ameshindwa kwenda na kasi
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. DK. John Pombe Magufuli
ambaye anataka kila fedha ya serikali ikusanywe na kuleta maendeleo kwa
watanzania wanyonge” Amesema Lukuvi.
Wakati huohuo Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amemuagiza Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk. Maulid Banyani kumpa
taarifa ya kiufundi na kitaalamu itakayokuwa imejitosheleza kuhusu
sababu za kuchelewa kumalizika kwa ujenzi wa Machinjio  ya Vingunguti
ambayo Rais. Dk. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi ukamilike Disemba
31 2019 wakati alipotembelea mradi huo.
Ameongeza kwamba sababu hizo
zielezwe wazi na ziwe ni za msingi ili baada ya hapo yeye amtaarifu Mh.
Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusu ucheleweshwaji huo kabla mwezi
januari mwaka ujao.
“Lazima nijiridhishe nione sababu
zenyewe kama ni za msingi, Kitaalam na Kiufundi ili nami nimtaarifu Ras
kuhusu kuchelewa kukamilika kwa mradi huu” Amesema Lukuvi.
Hata Hivyo Waziri Lukuvi
amelipongeza shirika hilo kwa utekelezaji wa mradi huo wa machinjio ya
Vingunguti kwa kasi na viwango vizuri ambao ni wa 35 kati ya miradi yote
ambayo Shirika la hilo linatekeleza nchi nzima ambapo amesema  mradi
huo unaendelea vizuri.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akiangalia leseni za wajasiriamali hao ambao wamepangishwa katika
nyumba ya NHC kinyume cha utaratibu kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo
Dk.Maulid Banyoni na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akimsikiliza  mmoja wa wapamgaji katika nyumba hiyo Said Seif Mketo
alipokuwa akimuelezea jinsi ambavyo wamekuwa wakinyanyaswa na mtu
aliyewapangisha kulia ni  Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid
Banyani.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akizungumza na  Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani
wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la machinjio ya nyama
Vingunguti ambalo linajengwa na NHC.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi huo
kulia ni  Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid
Banyani wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa machinjio hayo
Vingunguti.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *