Waziri lukuvi aokoa ardhi ya ajuza, aamuru kulipwa fidia ya milioni 500
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametoa miezi mitatu kwa wavamizi 110 waliovamia eneo la Ajuza Nasi Murio, mwenye umri wa miaka 98, lenye ukubwa wa hekari nane kumlipa kiasi cha sh. milioni 500 kama fidia.


Lukuvi ametoa agizo hilo Jijini Arusha Agosti 28, katika kata ya Sinoni ambapo amesema kila mtu atalipa fedha kulingana na ukubwa wa eneo alilopora.

Amesema serikali imewaonea huruma na kwamba watalipa shilingi 20,000 kwa kila mita moja za eneo.

Waziri amesema ili wavamizi hao waweze kurasimishwa na kuwa wamiliki halali watalazimika kulipa gharama za upimaji pamoja na gharama za kupata hati miliki pamoja na kodi ya ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *