Waziri mkenda apiga marufuku jeshi la polisi kukamata wafanyabiashara wa mazao

 

WAZIRI
wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda ,akizungumza na wananchi wa Sagara B kabla
ya kuanza ziara ya kutembelea Mashamba ya Kilimo cha Mkataba wa zao la
Mtama yanaliyolimwa katika wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.



Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Dk. Seleman Serera, ,akizungumza na wananchi wa
Sagara B wanaolima zao la Mtama wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.



Mwenyekiti
wa kijiji cha Sagara B, kilichopo wilayani Kongwa Bw.Gilbert
Mlwande,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda
mara baada ya kuzungumza na wananchi hao.



Wananchi
wa Sagara B wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda (hayupo
pichani)wakati ,akizungumza nao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea
Mashamba ya Kilimo cha Mkataba wa zao la Mtama yanaliyolimwa katika
wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.



WAZIRI
wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.
Seleman Serera wakitembelea Mashamba ya Kilimo cha Mkataba wa zao la
Mtama yaliyopo katika kijiji cha Nhumbi wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.



WAZIRI
wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda akizungumza na wananchi wa Ng’humbi
(hawapo pichani) mara baada ya kutembelea ya kukagua Mashamba ya Kilimo
cha Mkataba wa zao la Mtama yaliyopo katika kijiji cha Nhumbi wilayani
Kongwa Mkoani Dodoma.



WAZIRI
wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.
Seleman Serera ,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ng’humbi mara
baada Kutembelea na Kukagua Mashamba ya Kilimo cha Mkataba wa zao la
Mtama yanaliyolimwa katika kijiji cha Nhumbi wilayani Kongwa Mkoani
Dodoma.



Muonekano wa Shamba la Mtama lililopo katika kijiji cha Nghumbi wilayani Kongwa Mkoani Dodoma




Na.Alex Sonna,Kongwa


WAZIRI
wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda amepiga marufuku kwa jeshi la polisi
kukamata wafanyabiashara ya Mahindi wakati wanapeleka bidhaa yao sokoni
kwani hali hiyo inakatisha tamaa wakulima.


Prof.Mkenda
ametoa Kauli wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea
Mashamba ya Kilimo cha mkataba wa zao la mtama wilayani Kongwa.


Waziri
Mkenda amesema kuwa anatarajia kuzungumza na Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini (IGP) kuhakikisha Jeshi hilo linaachana na tabia ya
kukimbizana na wafanyabiashara hao wakati wakipeleka biashara zao
sokoni.


“Kuna
changamoto kubwa ya masoko inayowakabili wafanyabiashara wa mahindi
nchini, wafanya biashara hao wanauhuru wa kufanya biashara eneo lolote
nchini kwa kuwa wanakuwa wakitafuta masoko, hivyo kuwazuia na
kuwanyang’anya mazao yao wakati wakipeleka sokoni ni kuwavunja moyo na
kuwakatisha tamaa,”amesema Prof.Mkenda.


Hata
hivyo Prof. Mkenda amewataka askari wa Jeshi la Polisi nchini kuacha
tabia hiyo ya kuwanyanyasa na kuwasumbua wakulima na wafanyabiashara wa
zao hilo ambao
wanakuwa wakipambana kujikwamua na umaskini na kuchangia pato la taifa.


“Hiki
kitu kwa kweli sio kizuri hawa ni watanzania ambao wanatafuta masoko ya
zao hilo ni vema wakaachiwa ili kuendelea na biashara hiyo”amesema
Prof. Mkenda


Aidha
Waziri Mkenda amewataka maafisa ugani kuendelea kutoa elimu kwa
wakulima wa mazao mbalimbali wilayani humo ili wafanye kilimo chenye
tija ambacho kitaleta matokeo chanya kwao na taifa kwa ujumla.


Kwa
upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk. Seleman Serera, amesema wakulima
wa Kongwa wanashauku kubwa ya kuendesha kilimo cha mkataba cha zao la
mtama pamoja na kilimo cha mazao mengine kitaalamu ili kusonga mbele
katika kilimo.


Hivyo
Dk. Serera amesema ujio wa wawekezaji hao wa ndani kutawafanya
wakulima wa Kongwa kufanya kilimo cha kisasa ambacho kitaleta manufaa
makubwa kwa wakazi wa eneo hilo na taifa.


Awali
Mwenyekiti wa kijiji cha Sagara B, kilichopo wilayani Kongwa
Bw.Gilbert Mlwande amemshukuru Waziri huyo huku akisema amewasaidia
wakulima na wafanyabiashara kutatua changamoto ya kukimbizana na Jeshi
la Polisi Barabarani.