Waziri mkuchika azitaka taasisi zilizo chini ya ofisi ya rais kuwa mfano wa kuigwa kiutendaji na kimaadiliBaadhi ya Watumishi Waandamizi
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)
(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao chenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel S. Shindika
akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe.
George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) kwa kufanya ziara ya kikazi ya kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi
waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati
wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa chuo hicho.

Baadhi ya Watumishi Waandamizi
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)
(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao chenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua hoja za Watumishi Waandamizi
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa kikao
kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi
wa chuo hicho.


Na James K. Mwanamyoto
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika amewataka watumishi wa taasisi za
umma zilizo chini ya Ofisi ya Rais kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wa taasisi
nyingine za umma kiutendaji na kimaadili kwa kuwa jamii inaitazama Ofisi ya
Rais kama kioo cha utendaji kazi mzuri katika utumishi wa umma.
Waziri Mkuchika ametoa wito
huo wakati wa kikao kazi chake na Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania (TPSC) chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo
hicho.
Mhe. Mkuchika amewaasa watumishi
wa taasisi hizo kujiona kuwa ni sehemu ya kuitunza heshima ya Ofisi ya Rais kwa
kufanya kazi kwa uadilifu.
Amewasisitiza watumishi wa
chuo hicho kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano ili kuunga mkono
jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli za kuharakisha maendeleo ya nchi.
“Mimi nipo kwa ajili ya
kumsaidia Mhe. Rais ambaye ndiye Waziri wa Ofisi hii kusimamia utendaji kazi wa
taasisi zote zilizopo chini ya ofisi yake, hivyo hatuna budi kufanya kazi kwa
bidii, maarifa na weledi kama ambavyo yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kutekeleza
majukumu yake kwa vitendo”, amesisitiza Mhe. Mkuchika.
Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa
rai kwa Watumishi wa Umma wote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni,
Sheria, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi iliyopo ili kuepukana na vitendo vya
ubaguzi wa kijinsia, dini, ukabila na 
itikadi za kisiasa kwa wananchi na watumishi wenzao wanaowahudumia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo
na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel S.
Shindika kwa niaba ya chuo, amemthibitishia Mhe. Mkuchika kuwa, atahakikisha
maelekezo yote aliyoyatoa yanatekelezwa ili kuendana na kasi ya kiutendaji ya Mheshimiwa
Rais yenye lengo la kuleta maendeleo ya Taifa.