Waziri mkuu afiwa na kaka yake, awashukuru waliojitokeza mazishini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewashukuru watu wote waliojitokeza katika mazishi ya kaka yake Mzee
Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi (Jumatatu, Novemba 04, 2019)
nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila ‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa shukrani hizo leo
(Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika
kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema kwamba hayo ni mapenzi ya
Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia hiyo.
“Tulikuwa 12 na sasa tumebaki
watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba huu kwetu ni mkubwa
umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini hatuna namna ni
mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea kumuombea.
Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia, familia
imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.” 
Waziri Mkuu pia amemshukuru
Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole alizozitoa. “Jambo hili pia
limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye ametutaka tuwe watulivu katika
kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja kwa dhehebu lake aendelee
kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema.”
Amesema alipata taarifa za
msiba huo wakati akijiandaa kwenda wilayani Ruangwa kwa ajili ya
kushiriki mazishi yamwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa
Wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani Mmuya. 
Kwa upande wake, Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Ven
ance Mabeyo akitoa salamu za
pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na 
Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na majonzi waliyonayo kwa
kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa
ndiye anayetoa na anayetwaa. 
“Hakuna namna ya kurekebisha maamuzi ya
Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu kwa sala Mwenyezi Mungu
ampokee kwa amani.”
Naye, Mwakilishi wa Mufti na
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo amesema amewataka wananchi
wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni kawaida kwa binadamu kujisahau
lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya kutukumbusha juu ya uwepo
wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale yalikuwa ya wajibu
kuyatekeleza.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *