Waziri mkuu amwakilisha rais magufuli katika mkunao wa 18 wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (nam)

WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2019 anatarajiwa kumwakilisha Rais
Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na
Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na
kwingineko duniani utakaofanyika Baku, Azerbaijan.


Mkutano
huo unalenga kujadili namna ya kutatua changamoto za kisiasa, kiuchumi
na kijamii zinazokabili nchi wanachama wa NAM katika nyakati za sasa,
pamoja na na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi
wanachama wa umoja huo.

Waziri
Mkuu aliwasili nchini Azerbaijan jana (Ijumaa, Oktoba 25, 2019) na
alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Bw. Ali Ahmadov pamoja
na viongozi wengeine wa Serikali hiyo. Mapokezi hayo yalifanyika katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heydar Aliyev.

Ajenda
za mkutano huo ni kupokea ripoti za mkutano wa maandalizi wa Mawaziri,
kupokea ripoti ya mkutano wa maandalizi wa Maafisa Waandamizi, uchaguzi
wa nchi zitakazokuwa wajumbe katika ofisi ya uratibu wa shughuli za NAM,
New York kwa kipindi cha mwaka 2019-2022.

Mbali
na ajenda hizo, pia ajenda nyingine za mkutano huo ni kupokea ripoti za
shughuli za umoja huo zilizotekelezwa chini ya Mwenyekiti wa NAM,
Venezuela, mjadala mkuu, pamoja na kupitisha maandiko yatokanayo na
mkutano.

Mheshimiwa
Majaliwa ameambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirkiano wa
Afrika ya Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro na Balozi wa Tanzania Nchini
Urusi ambale pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon
Mumwi.

Awali,
Waziri Mkuu alikuwa Sochi nchini Urusi ambako pia alimwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Uchumi kati ya Urusi na Afrika
(Russia – Africa Economic Forum) na baadae Mkutano wa wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa Mataifa ya Afrika uliofunguliwa na Rais wa Urusi Vladimir
Putin.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAMOSI, OKTOBA 26, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *