Waziri mkuu atembelea banda la tanzania la maonesho ya ticad 7


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Bi. Edda Magembe, Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japan alipotembelea banda la maonesho ya vivutio vya utalii wa Tanzania jijini Yokohama, Japan tarehe 28 Agosti 2019. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini Japan akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Maonesho hayo yanaenda sambamba na mkutano huo ambao umetoa fursa kwa nchi za Afrika kujitangaza kwenye masuala ya vivutio vya utalii, uwekezaji na biashara.

Mhe. Waziri Mkuu akisalimiana na mmoja wa washiriki kwenye banda la maonesho la Tanzania. Maonesho hayo yanafanyika sambamba na Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7)

Waziri Mkuu akiangalia moja ya kipeperushi kuhusu maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini alipotembelea banda la Tanzania kwenye Mkutano wa TICAD 7 unaofanyika jijini Yokohama, Japan

Waziri Mkuu akiangalia moja ya bidhaa zinazopatikana nchini alipotembelea banda la Tanzania

Waziri Mkuu kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa maonesho kwenye banda la Tanzania yanayoendelea sambamba na Mkutano wa Saba wa TICAD

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *