Waziri mkuu mgeni rasmi baraza la maulidi, atoa ng’ombe watano wa kitoweo

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Kassim ametoa ng’ombe watano kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya sherehe za Maulidi.
Ng’ombe hao wa kitoweo walikabidhiwa juzi kwa kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke na Mkuu wa Mkoa huo John Mongela kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Akizunguza wakati akikabidhi ng’ombe hao kwenye Vviwanja vya Furahisha, Kata ya Kirumba katika Manispaa ya Ilemela zinakofanyikasherehe hizo kitaifa,  Waziri Mkuualisema kitoweo hicho kitawasaidia Waislamu katika kipindi hiki cha kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W.
Kaimu sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, alhaji Hassani Kabeke akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kukabidhi kitoweo kwa waumini wa dini hiyo kwa ajili ya maulidi lakini pia saruji ya ujenzi wa msikiti jijini humu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Furahisha Kirumba, Manispaa ya Ilemela kabla ya kuwakabidhi ng’ombe watano wa kitoweo waliotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim lakini pia mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Bakwata mkoani huu jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela,wa tatu kutoka kushoto akitoa neno wakati wa kukabidhi ng’ombe watano wa kitoweo waliotolewa kwa BAKWATA mkoani hapa kwa ajili ya sherehe za maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W yanayofanyika kitaifa Mwanza, Novemba 9.

Waziri Mkuu aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu wanaposherehekea maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume wahakikishe wanadumisha mshikamano,amani na utulivu wa nchi, tunu pekee inayoliliwa na mataifa mengi duniani.
“Niwatakie sherehe na maadhimisho mema ya maulidilakini jambo pekee na muhimu tuhakikishe tunafanya kwa utulivu, amani na mshikamano,ingawajambo hili kubwa ni  kuwajenga watu kirohona kiimani,”alisema.
Sheikhe Kabeke akizungumza baada ya kupokea kitoweohicho kwa niaba ya BAKWATA na waislamu, alisema kitoweo hicho ni kafara njemaisiyo na doa.
  “Serikali haina dini, ni faraja kwetu sisi Waislamu kutuunga mkono kwa kitoweo hiki ambacho ni kafara kubwa.Hii ndiyoserikali tunayoitaka na Tanzania tunayoifahamu ya watu wenye ukarimu,”alisema.
Alimshukuru Waziri Mkuu pamoja na serikali kwa kutambuamahitaji ya waislamu katika kipindi hikina kuamua kuwasaidia kitoweo kitakachowawezeshakutimiza jambo hilo la maulidi bila shida.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Maulidi litalofanyika jijini Mwanza baada ya sala itakayoswaliwa kwenye viwanja vya Furahisha.

Waziri Mkuu atawasili jijini Mwanza jioni kwa ajili ya shughuli hiyo akiungana na Waislamu wa jiji hilo na Watanzania wengine katika kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W