Waziri mkuu wa lesotho pamoja na mkewe wakabiliwa na tuhuma za mauaji

Waziri
Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane pamoja na mkewe, Maesaiah Thabane
wanatakiwa kuhojiwa kuhusiana na mauaji yaliyotokea mwaka 2017 ya Mke wa
kwanza wa Thabane, Lipolelo Thabane (58)

 

Lipolelo
alikuwa ametengana na mume wake na alikuwa akiishi peke yake tangu
mwaka 2012 ambapo aliuawa siku 2 kabla ya Thabane kuapishwa kuwa Waziri
Mkuu kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake

Ushahidi
wa hivi karibuni uliowasilishwa Mahakamani na Kamishena wa Polisi
umebaini kwamba kulikuwa na mawasiliano ya simu katika eneo la tukio kwa
kutumia namba ya simu inayodhaniwa kuwa ni ya Thabane

Waranti
ya kukamatwa kwa Maesaiah Thabane ilishatolewa lakini hajaonekana
hadharani kwa wiki 2 sasa, hakuna anayejua alipo na Thabane amekataa
kusema alipo mke wake