WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020/2021
umelenga kutekeleza maeneo ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na
kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuweka mkazo
katika upatikanaji wa huduma bora za jamii ikiwemo elimu, maji, afya,
umeme na barabara.
Ametaja
maeneo mengine ni ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda kwa kuimarisha
sekta ya kilimo kwa kujenga viwanda vitakavyotumia malighafi
inayopatikana nchini, kuimarisha mashirika ya viwanda na kuanzisha na
kuendeleza maeneo ya viwanda.

Waziri
Mkuu ameyasema hayo jana (Ijumaa, Novemba 15, 2019) wakati akiahirisha
mkutano wa 17 wa Bunge la 11 jijini Dodoma. Amewasisitiza wananchi
kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kuiwezesha
nchi kufikia malengo ya kujenga uchumi imara, unaojitegemea na wenye
kuweza kuhimili ushindani.

“Ujenzi
wa mazingira wezeshi katika kuendeleza miundombinu itakayosaidia
maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini; kuhakikisha Watanzania wenye
sifa stahiki wanapewa kipaumbele katika kandarasi au ajira zinazotokana
na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.”

Amesema
eneo lingine ni kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa Mpango. Baada ya
tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano 2016/2017–2020/2021 kwa lengo la kuimarisha usimamizi na
kuanza maandalizi ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano (2021/2022–2025/2026).

Kadhalika,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kusisitiza Maafisa Masuuli wazingatie
maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo na wahakikishe kamati za mipango na bajeti katika mafungu yao
zinatekeleza majukumu yake ipasavyo. “Serikali kwa upande wake itaandaa
mipango ya kisekta, kitaasisi na kimaeneo ambayo utekelezaji wake
utachochea ujenzi wa uchumi wa viwanda, mageuzi ya uchumi na maendeleo
ya watu.”

“Katika
udhibiti wa matumizi, naendelea kuwasisitiza Maafisa Masuuli
wahakikishe wanatumia mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma
(Tanzania National Electronic Procurement System – TANePS). Hivyo, kila
taasisi ya nunuzi ihakikishe inatumia mfumo huo kabla ya tarehe 31
Desemba 2019.

Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa upande wake itaendelea kufanya maboresho makubwa
katika sekta zinazogusa wananchi moja kwa moja na kuhakikisha kuwa
matunda ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi.

“Watanzania
wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, katika kipindi hiki ambacho amekuwa akichukua hatua za
makusudi kuhakikisha anajenga uchumi imara, kuboresha kipato na hali ya
maisha ya wananchi.”

matunda ya maboresho hayo yanayoendelea yanaonekana katika maeneo
mengi. “Ndani ya miaka 26 kuanzia 1991/1992 hadi 2017/2018 kiwango cha
umaskini wa mahitaji ya msingi kimeweza kupungua kwa asilimia 13.
Kadhalika, umaskini wa chakula nao umepungua kutoka asilimia 10 mwaka
2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18.”

Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amesema katika kuelekea msimu wa kilimo wa
2019/2020 hali ya upatikanaji wa chakula nchini imeendelea kuimarika
kutokana na uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula kwa msimu 2018/2019,
ambao ulifikia tani milioni 16.41 ikilinganishwa na mahitaji ya tani
milioni 13.84 na kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula
kwa asilimia 119.

pamoja na uzalishaji huo mzuri, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya
nafaka katika baadhi ya maeneo kutokana na hali ya mvua kutokuwa nzuri
na kuwepo kwa dalili za kupanda bei za nafaka, Serikali imetoa maelekezo
kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa kuhakikisha inasambaza nafaka
kwenye maeneo yenye upungufu ili kukabiliana na changamoto ya kupanda
kwa bei.

“Nitumie
fursa hii kuwahimiza wakulima kutumia vizuri mvua za vuli zinazoendelea
kunyesha maeneo mengi ya nchi yetu kwa kupanda mazao yanayostahimili
ukame na ekolojia ya maeneo husika. Aidha, tukumbuke pia kujiwekea akiba
ya kutosha ya chakula kwa ajili ya matumizi ya kaya baada ya mavuno
badala ya kuuza chakula chote.”

Kuhusu
upatikanaji wa pembejeo, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha
wakulima wanapata mbolea kwa wakati na bei nafuu, Serikali imetoa bei
elekezi kwa mbolea aina ya DAP na UREA ambazo zipo katika Mfumo wa
Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja. “Hivyo, nitumie fursa hii kuzikumbusha
mamlaka husika kuhakikisha kwamba bei elekezi zinafahamika kwa wakulima
katika maeneo yote na wauzaji wanauza kwa kuzingatia bei hizo.”

Pia,
Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu masoko ya mazao ya kilimo ambapo
amesema licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini,
kumekuwepo na changamoto kadhaa za upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa
baadhi ya mazao ikiwemo la pamba, korosho na tumbaku.

changamoto hizo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko na
mwenendo wa bei katika soko la dunia pamoja na uwezo mdogo wa kuchakata
mazao hayo nchini, hivyo Serikali inaimarisha mifumo ya masoko ya mazao
ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza tija na kupunguza gharama za
uzalishaji kwa kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo
na uvuvi.

“Hatua
hizi zitasaidia kuongeza thamani ya mazao na hivyo, kuimarisha bei. Kwa
sasa tunaendelea na msimu wa mauzo wa zao la korosho baada ya mazao ya
pamba na kahawa kumaliza. Minada ya korosho inaendelea vizuri. Viongozi
wa Mikoa na Wilaya wasimamie malipo kwa wakulima na kuhakikisha
wanalipwa kwa wakati.”