Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi Lugola akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi uwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa majeshi ya Polisi za nchi za ukanda wa mwa Afrika(EAPCCO) katika kikao cha 19 cha baraza la mawaziri kilichofanyika Jijini Arusha
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AKABIDHIWA UENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI EAPC
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi Lugola amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa majeshi ya Polisi za nchi za ukanda wa mwa Afrika(EAPCCO) katika kikao cha 19 kilichofanyika Jijini Arusha leo sep20 kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani wa nchi ya Sudani ambapo amewakilishwa na Luteni Jeneral wa Polisi Adil Mohamed
Akizungumza baada ya kukabidhiwa uwenyekiti Waziri Lugola amesema kuwa anaahidi kufanyia kazi na kuzingatia maagizo yote yanayotakiwa kutekelezwa na kuendeleza mafanikio ya kuondoa changamoto zinazokabili ukanda wa Afrika.
Amesema kuwa yapo makubaliano ya msingi ambayo wamekubaliana katika mkutano ambayo yanazitaka nchi wanachama kupitia EAPCCO kuendelea kujipanga kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kama vile ugaidi,utakatishaji wa fedha haramu,wizi wa magari,biashara haramu ya dawa za kulevya,usafirishaji wa binadamu,uuzaji na usafirishaji wa silaha uhalifu wa ujangili na uharamia,pamoja,uhalifu mwingine.
Amewahakikishia wananchi wa nchi zote hizo 14 kuwa msingi mkubwa wa ustawi wa maisha ni msingi mkubwa wa maendeleo ya wanadamu ikiwa ni pamoja na maisha ya wananchi na mali wanahitaji kuhakikishiwa ulinzi na majeshi hayo ya polisi katika nchi wanachama.
Katibu mtendaji wa Interpol Jurgen Stock amesema wao wataendelea kutoa ushirikiano na kuangalia namna ambavyo watapambana na uhalifu wa kimtandao na ugaidi haswa katika ukanda wa Mashariki sambamba na kupambana na rushwa na uhalifu unaovuka mipaka.
Amesema kuwa Mfumo wa mawasiliano umeweza kuwagharimu zaidi dola mil 99 kwaajili ya kuangalia nini kinachoendelea katika nchi za ukanda wa Mashariki na namna tunavyoweza kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa tunakuwa na mfumo wa kutoa taarifa kwa pamoja .
Stock amesema kuwa ushirikiano unahitajika katika nyanja zote ikiwemo mafunzo ya watendaji,haswa mafunzo maalum ,makosa yanavyovuka mipaka ,operesheni za pamoja kufanya upelelezi wanpamoja wa kubaini taarifa za kiitelijensia.
Akisoma risala ya kufunga kikao hicho cha Mawaziri wa EAPCCO Lugola amelishukuru Baraza hilo la Mawaziri kwa kumuamini na kumchagua kuwa mwenyekiti kwa mwaka 2019-2020 amewaomba nchi wananchama kuendeleza ushirikiano sambamba na kuwa na utashi wa kusiasa.
Amesema kuwa katika ukanda wa mashariki kuna changanoto mbalimbali za uhalifu,maeneo ya msingi ni kuwajengea watendaji wao uwezo huku akiwataka viongozi wa Askari kuimarisha nidhamu kazini sambamba na kuepuka visingizio.