Zahanati ya duce waboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


 

Chuo
Kishiriki cha Elimu Dar es  Salaam (DUCE) kimezindua jengo jipya la
Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es
Salaam.


 


Jengo
hilo limezinduliwa na Mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora
Aminiel Nnko litakalokuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za Afya ya uzazi
na mtoto.


 


Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa jengo hilo, Aimbora amesema DUCE wamefanya jambo
kubwa sana kwani afya ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo katika taifa
letu.


 


Aimbora
amesema, zahanati ya DUCE imekuwa inatoa huduma nzuri sana kwa jamii
inayowazunguka na hata yeye ni mmoja wa watu wanaofika kupata huduma
hapo.


 


Amesema,
kutanua wigo kwa kuweka huduma ya Afya ya uzazi na Mtoto itawasaidia
kuanzia watumishi wa Chuo, wanafunzi na hata wananchi wanaokaa kwenye
mazingira yanayowazunguka.


 


“Mmefanya
jambo kubwa kutanua wigo wa huduma kwani ni jambo kubwa na la muhimu,
kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya tunawapongeza sana na mmesema mnataka
kuongeza hadhi ya Zahanati ninaamini hilo litafanikiwa kwa juhudi kubwa
mnazofanya,”amesema Aimbora.


 


“Niwapongeze
zaidi kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli za
kutekeleza na kujenga Zahanati ili wananchi wapate huduma nzuri, pia
madaktari na waaguzi mnafanya kazi kubwa ya kutoa huduma bora ya Afya,”


 


 


Naye
Mkuu wa Chuo Kishiriki RASI Prof Bernadeta Killian amesema katika
kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2019, zahanati ya DUCE imeweza
kuwahudumia wagonjwa 15,138 wakiwemo wanafunzu, watumishi na wakaazi
wanaozunguka maeneo hayo.


 


Amesema,
kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya ya uzazi na mtoto kwa wana
DUCE na wanajamii wanaoishi jirani imewasukuma kujenga jengi hilo ili
kuwezesha huduma inapatikana na kuongeza wigo na kipato kwa chuo.


 


“Jumla
ya Milion 59 zimetumika kukamilisha jengo, Milion 41.7 zimetumika
kukamilisha ujenzi wa jengo hilo na Milioni 17.3 kwa ajili ya kununulia
thamani na zote zimetokana na mapato ya ndani ya chuo, “amesema Rasi
Bernadeta.


 


“Chuo
kina mikakati endelevu ya kuiboresha Zahanati ili iweze kutoa huduma
bora zaidi ksa wanajumuiya ya DUCE na wananchi kwa ujumla na mikakati
hiyo ikiwa ni kupandisha hadhi Zahanati kuwa kituo cha Afya, kuanzisha
kamati ya Afya ya Chuo, kuifanya zahanati kuwa kliniki ya huduma za
kibingwa na kutangaza huduma kwa watu wengi zaidi,” 


 


Katika
jengo hilo, Kumepatikana chumba kimoja cha Daktari kitakachotumika
kutolea huduma za matibabu kwa wagonjwa wote, na itasaidia kupunguza
changamoto ya vyumba.


 


Pia,
kutakuwa na huduma ya ufuatiliaji wa ukuaji bora na wenye afya kwa
watoto chini ya miaka mitano sambamba na utoaji wa chanjo kwa watoto hao
hali kadhakika kutakuwepo na utoaji wa huduma rafiki kwa vijana.


Mkuu
wa Chuo Kishiriki (DUCE) RASI Prof Bernadeta Killian akisoma hotuba kwa
mgeni rasmi yw uzinduzi wa jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika
zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.Mwakilishi 
wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akitoa pongezi kwa Chuo
Kishiriki DUCE kwa hatua kubwa waliyoifanya ya kujenga jengo jipya
litakalokuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za Afya ya uzazi na mtoto.Mwakilishi 
wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akizindua jengo jipya la
afya ya Mama na Mtoto litakalotoa huduma kwa watumishi wa Chuo
Kishirikishi DUCE, wanafunzi na wakazi wa maeneo hayo.
Mwakilishi 
wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akipata maelezo kutoka
kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya DUCE Dr Saning’o Sangeti baada ya
kuzindua jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo
hicho leo Jijini Dar es Salaam.Naibu
Rasi (Utawala)  Dkt  Method Semiono akitoa neno la Shukrani kwa
Mwakilishi wa Mkuu ws Wilaya baada ya kuzindua jengo jipya la Afya ya
uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja baada ya uzinduzi wa Jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto
katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.