Zaidi ya shilingi milioni 154 zatumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa,ukarabati wa shule wilayani tandahimba

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akizindua madarasa hayo akiwa na wafadhili waliowezesha mradi huo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba na Mwenyekiti wa Eclat wakisaini makabidhino hayo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akikabidhi hati ya makabidhino Afisa Elimu Msingi Wilaya Hadija Mwinuka
 Matundu ya Choo kwa ajili ya wanafunzi na walimu Wao
Meneja wa mradi Msham Bashir (mzawa qa Luagala)ambaye ndiye aliwashawishi kuja kuboresha miundombinu ya Elimu Wilayani hapo
 Shule ya msingi Luagala ‘B’ katika muonekano mpya
 Wananchi wa Kijiji Cha Luagala ‘B’wakishuhudia uzinduzi wa shule


****
Zaidi
ya shilingi Milioni 154 zimetumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa
na kukarabati shule ya Msingi Luagala ‘B’ Wilayani Tandahimba

Akizindua
madarasa hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba amesema
madarasa hayo yamewekwa na madawati tayari kwa wanafunzi kuendelea na
masomo

“Tumezindua madarasa haya lakini pia wametukabidhi shule
ikiwa katika muonekano unaovutia  ambapo kazi hii imefanywa na taasisi
ya Eclat na Upendo ,”amesema Waryuba

Naye Mwenyekiti wa taasisi
ya Eclat Toima Kiroya ameeleza kuwa katika mradi huo wameweza kujenga
vyumba vitatu vya madarasa,kukarabati majengo 8,kisima chenye ujazo wa
Lita 150,000,matundu 16 ya Choo,madawati 65,meza za walimu 16 na viti 16

Hata
hivyo Dk Fred Heimbach wa Upendo Society kutoka Ujerumani ameeleza kuwa
madhumuni ya ushirika huo ni kuboresha miundo mbinu katika sekta ya
elimu

Sambamba na Hilo  Meneja wa mradi huo Msham Bashir
ameishukuru serikali kwa kushirikiana  kuanzia ngazi ya Kijiji hadi
Wilaya hivyo wananchi wanajukumu lankutunza miundo mbinu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *