Zao la mpunga na mahindi kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani

NA SALVATORY NTANDU

Serikali
nchini imeviagiza vyama vikuu vya ushirika kuhakikisha wanawauganisha
wakulima wa zao la mahindi na Mpunga katika ushirika ili kuongeza
mnyororo wa thamani wa mazao hayo ili kuanzia mwakani 2020 yaanze kuuzwa
kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Kauli hiyo imetolewa Disemba 28 mwaka huu na Naibu waziri wa Kilimo
Hussein Bashe wakati akizungumza na wakulima wa zao la tumbaku na pamba
katika mkutano mkuu wa 24 wa chama cha Ushirika kahama (KACU)
uliofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rai Dk John Pombe
Magufuli imedhamiria kumkomboa mkulima kwa kuhakikisha ananufaika na zao
analozalisha hivyo ni budi kuanza haraka mchakato wa kuwaunganisha
wakulima wa mazao ya mahindi na Mpunga katika Ushirika.
“Haiwenzekani wakulima wetu  wa mpunga wananyonywa wa walanguzi wa
mazao, gunia moja la mpunga wakati wa mavuno linauzwa elfu 35 na
likiwekwa gahalani na wafanyabiasha mwezi disemba kama huu bei yake
hupanda na kufikia shilingi laki mmoja na thelathini ndio maana tunataka
waaingizwe kwenye ushirika”alisema Bashe.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi, Zainab Telack alisema zao
la mpunga na mahindi liingizwa katika mfumo wa ushirika wakulima
watanufaika kwa kuuza mazo yao kwa bei ya juu ilikinganishwa na sasa
ambapo wanalazimika kuuza kwa bei zisizo rasmi.
“Halmashauri zetu zitaongeza mapato kutokana kodi za  uuzwaji wa mazao
haya ambayo awali yalikuwa hayapewi kipaumbele kama vile tumbaku na
Pamba zilizokuwa zinasimamiwa na vyama vya Ushirika”alisema Telack.
Telack pia aliwataka wakulima wa mpunga na mahindi kujikita na kilimo
cha umwagiliaji kwa kujenga mabwawa ya maji ili kuvuna maji ambayo
yanapatikana kwa wingi katika msimu huu wa masika ambayo wataweza
kuzalisha tena zao hilo kindi cha kiangazi na kupata faida mara mbili.
Nae Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Emanuel
Charahani alisema watahakikisha wanatekeleza agizo hilo ili wakulima wa
mazao hayo waweze kupata faida kutokana na kilimo wanachozalisha ili
kundokana na kuwanufaisha wafanyabiashara ambao wananunua mazo yao
katika masoko ambayo sio rasmi.
sambamba na hilo Charahani amewataka viongozi wa vyama vyote vya
ushirika nchini kuanzisha mfuko wa pembejeo ambao utakuwa na jukumu la
kununua pembejeo zote za wakulima na  kuondokana na utegemezi wa kukopa
fedha kwenye mabenki ambazo riba zake ni kubwa.
Paschal Robart na Rehema Shabani ni  miongoni mwa  wakulima wa zao la
Tumbaku kutoka Halmashauri ya Ushetu walisema ushirika umesaidia
wakulima wengi kupata faida kutokana na kuuza mazao yao kwa bei ya juu
hivyo kujumuishwa kwa mazao ya mahindi na tumbaku kutaongeza vipato vya
familia zao.
Mwisho.