Zoezi la uandikishaji orodha ya wapiga kura uchaguzi serikali za mitaa waongezewa siku tatu hadi oktoba 17, 2019

  
  
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA
RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

 


 TANGAZO LA MAREKEBISHO YA RATIBA YA
UANDIKISHAJI WA ORODHA
 
YA
WAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA
2019  
 

(Limetolewa chini ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
za Mwaka mwaka
2019  (Matangazo ya Serikali Na 371, 372, 373 na 374 ya
mwaka 2019).
Kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za
Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo (Tangazo la
Serikali Na. 371 la mwaka 2019), Kanuni ya 51 ya Kanuni za Uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya 
Mtaa katika Mamlaka za Miji
(Tangazo la Serikali Na. 372 la mwaka 2019), Kanuni ya 52 ya Kanuni za Uchaguzi
wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa
Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 373
la mwaka 2019) na Kanuni ya 52 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji,
Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji
za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 374 la mwaka 2019) Waziri mwenye dhamana
ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa. 
Tangu tarehe 8 Oktoba, 2019
kumekuwa na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika Orodha ya Wapiga Kura
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba,
2019.
 
Zoezi la uandikishaji lilipangwa
kumalizika tarehe 14 Oktoba, 2019.  Zoezi
hili limeendelea kupata mafanikio makubwa kwani hadi mnamo tarehe 12 October
zaidi ya wananchi milioni kumi na moja waliweza kujiandikisha katika daftari la
Orodha ya Mpiga Kura za Serikali za Mitaa.
Hata hivyo, kumejitokeza changamoto kuu mbili wakati zoezi la
uandikishaji likiendelea. Changamoto hizo ni kama ifuatavyo;
1.    Kumekuwa
na mvua nyingi kwa Mikoa  mingi hivyo
kusababisha watu wengi kushindwa kujiandikisha kwa wakati. Maeneo mengine
baadhi ya kaya zimejikuta zimezingilwa na maji hususani kwa Mkoa wa Morogoro na
baadhi ya maeneo ya Mikoa ya ukanda wa Pwani. 
2.    Baadhi
ya wananchi ambao zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
limewapitia hivi karibuni au limekuwa likiendelea katika maeneo yao wamekuwa
kichanganya kwamba kwakuwa wamesha jiandikisha katika daftari la kudumu na
kupewa kitambulisho cha Mpiga kura wamekuwa na dhana isiyo sahihi kwamba
vitambulisho hivyo vitawawezesha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa hata kama hawata jiorodhesha katika daftari la orodha ya mpiga kura kwa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Dhana hiyo imesababisha baadhi ya wananchi
kuchelewa kujiandikisha katika zoezi linalo endelea sasa la uandikishaji
kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 Kutokana na changamoto hizi kuu mbili, na
kutokana na misingi ya utoaji  wa haki na
kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama zilivyo
ainishwa hapo juu natoa Mwongozo kuwa zoezi la uandikishaji linaongezewa siku
tatu zaidi za uandikishaji hadi tarehe 17 Oktoba, 2019 badala ya tarehe 14
Oktoba, 2019 iliyotangazwa awali. 
Kufuatia mabadiliko
hayo, ratiba ya uandikishaji wa Orodha ya Wapiga Kura na matukio yanayohusu
uandikishaji yatakuwa kama ifuatavyo:
Na.  
TUKIO  
TAREHE  
MHUSIKA  
1.  
Zoezi la uandikishaji wa
wapiga kura   
 
8-17 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
2.  
Kubandikwa kwa Orodha ya
Wapiga Kura
 
18 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
3.  
Ukaguzi wa Orodha ya
Wapiga Kura  
 
18-24 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
4.  
Pingamizi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura    
18-24 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
5.  
Uamuzi kuhusu pingamizi    
24-25 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
6.  
Marekebisho ya Orodha ya Wapiga Kura    
24-25 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
Msaidizi  
7.  
Kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi
 24-26 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
  
Uamuzi wa rufaa  
24-29 Oktoba, 2019  
Msimamizi wa Uchaguzi  
  
Matukio mengine
ya Uchaguzi hayataathiriwa na mabadiliko haya. 
Kwa Tangazo hili, Wananchi wote
wanaombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kura
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya  kupiga kura katika Uchaguzi huo.  

SELEMANI
S. JAFO (MB)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS,
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

13 Oktoba, 2019