Kipchoge mkenya mwenye asilia ya longido nchini tanzania aweka historia mpya ya dunia


EMMANUEL MBATILO

Mwanariadha kutoka nchini Kenya
mwenye asilia ya Longido nchini Tanzania Eliud Kipchoge amekuwa mwanariadha wa kwanza duniani kutumia chini ya
saa 2 kumaliza mbio za marathon (Kilomita 42).

Mwanariadha huyo ametimiza ndoto
yake na kuweka rekodi mpya ya dunia leo nchini Austria akitumia saa 1,
dakika 59 na sekunde 40.2 (1:59:40.2) kwenye mashindano maalum ya INEOS
1:59 Challenge.

Kipchoge amevunja rekodi yake binafsi ya kutumia saa 2:01::39 aliyoiweka mwaka jana kwenye Marathon ya Berlin.
Tanzania inajivunia mwanariadha huyu kutokana na umahiri wake wa kukimbia katika ukanda wa Afrika Mashariki.