Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kutumia mashindano ya shimuta kuhamasisha utalii wa ndani

 

MAMLAKA
ya Hifadhi ya Ngorongoro wamesema kwamba watatumia mashindano ya
Shimuta yanayofanyika Jijini Tanga kama sehemu ya kuhamasisha utalii wa
ndani.

Hayo yalisemwa na Kiongozi wa michezo wa Mamlaka hiyo na
Mjumbe wa kamati tendaji ya Shimuta, Marcel Kitulo mjini hapa ambapo
alisema wamekuja kushiriki wakiwa wamebeba ujumbe wao shughuli zao ni za
utalii.

Alisema hivyo watahamasisha pia kutembelea vivutio vya
utalii ikiwemo Mapango ya Amboni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
ikiwemo kuwaeleza mazuri ya ngorongoro.

“Tutatumia mashindano
hayo ya Shimuta kama sehemu ya kuhamasisha wafanyakazi kufanya utalii wa
ndani kutembelea vuvutio vyetu ikiwemo Mapango ya Amboni na Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro”Alisema

Aidha alisema kwamba mashindano
hayo yamekuwa yanakua kutokana na timu kuongezeka kila mwaka na hivyo
kuongeza mwamko na ushindani pia

Hata hivyo alisema kwamba wao
wamefika kushiriki lakini pia kama wadhamini wa mashindano hayo kutokana
na kusaidia baadhi ya mahitaji muhimu shimuta na wamekuwa wakifanya
hivyo mara kwa mara.

Alisema pia wao wanashiriki kujenga afya za
wafanyakazi kwa sababu mashindano hayo ni zaidi ya michezo ya uwanjani
yanatoa fursa wafanyakazi kutengeneza mtandao kwa wafanyakazi wa umma na
makampuni binafsi.