Simba kutoa tamko leo kuhusu tuhuma za mchezaji wa yanga, ramadhan kabwili

Uongozi
wa Simba umesema kuwa leo utalitolea ufafanuzi suala la madai ya mlinda
mlango wa Yanga, Ramadhan Kabwili kudai kuwa aliahidiwa gari aina ya
Toyota IST endapo angefanya makusudi ya kutocheza mchezo wao wa msimu
uliopita 2018/19.


Kabwili
alidai kuwa, kuna watu ambao anadai walikuwa ni viongozi wa Simba
walimfuata na kumtaka afanye makusudi kwenye mechi zake apate kadi ya
njano ili asipangwe kwenye kikosi kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za
njano.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watajibu tuhuma alizotoa mchezaji huyo ila cha msingi awe na ushahidi.


Tutajibu tuhuma za jumla jumla alizotoa huyu mchezaji kwa klabu yetu.
Muhimu wakati huu akijiandaa kikamilifu na ushahidi wa hizo tuhuma,” .