Mabingwa watetezi, Simba SC leo
wameiadhibu Ruvu Shooting baada ya kuichapa mabao 3-0 katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni
mshambuliaji Miraji Athumani ‘Madenge’ aliyefunga mabao mawili, huku
lingine likifungwa na beki Mbrazil, Tairone Santos da Silva.

Na kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi
wanafikisha pointi 25 katika mchezo wa 10 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu
ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye pointi 23 za mechi 11, wakati Ruvu
Shooting inabaki pointi zake 15 baada ya kucheza mechi 12.

Miraj anayefahamika pia kwa jina la
utani Sheva akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa
Ukraine, Andriy Mykolayovych Shevchenko alifunga bao la kwanza dakika ya
39 kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia Shomari Kapombe.

Beki Mbrazil, Tairone Santos da Silva
aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka Atletico
Cearense ya Daraja la Nne nchini kwao akafunga bao la pili dakika ya 47
akimalizia mpira wa kona wa kiungo Mkenya, Francis Kahata kutoka kulia.

Miraj aliyeibukia timu ya vijana ya
Simba, maarufu kama Simba B kabla ya kwenda kujikomaza kisoka Mwadui FC
ya Shinyanga, Toto African ya Mwanza na Lipuli FC ya Iringa kisha
kurejea nyumbani msimu huu, alifunga bao la tatu kwa shuti dakika ya 74
akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda Meddie Kagere.

Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa;
Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Renatus Ambroce,
Rajab Zahir, Zuberi Dabi, Emmanuel Martin, Shaaban Msala/Moses Shaaban
dk73, Saadat Mohamed, Said Dilunga/Fully Maganga dk58 na Edward
Christopher/Abdulrahman Mussa dk61.

Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe,
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos, Pascal Wawa, Gerson Fraga
‘Viera’, Hassan Dilunga/Deo Kanda dk63, Muzamil Yassin, Meddie
Kagere/Ibrahim Ajibu dk75, Miraji Athuman ‘Madenge’ na Francis
Kahata/Sharaff Eldin Shiboub dk79.

Chanzo – Binzubeiry blog