Simba yawatwanga mashujaa nyumbani

Bao pekee la Simba SC kupitia kwa Sharaf Shiboub mnamo dakika ya 56
kipindi cha pili, limeipa ushindi timu hiyo dhidi ya Mashujaa FC katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma.





Simba imecheza mechi yake ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara msimu huu.





Katika mchezo huo, uwanja wa Lake Tanganyika ulionekana kuwa na
changamoto haswa kwa Simba kutokana na vipara vingi na sehemu kadhaa
zikiwa hazina nyasi.





Mapema baada ya mechi kumalizika, Beki Yusuph Mlipili, amesema wangeweza
kushinda zaidi ya bao tatu lakini uwanja ulikuwa shida kwao.







“Uwanja kwakweli upande wetu ulikuwa na changamoto nyingi.







“Tungeweza kushinda zaidi ya bao tatu, hii imepelekea tushindwe kucheza
kama ambavyo tumezeoa kucheza siku zote,” amesema Mlipili.