Wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mashindano ya mbio za mita 1500 katika viwanja vya Chuo cha Walimu leo Juni 14, 2021 mjini Mtwara.
Mratibu wa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Leonard Thadeo akitoa maelekezo kwa waamuzi na waratibu wa michezo wa mikoa mbalimbali iliyoshiriki mashindano hayo leo Juni 14,2021 mjini Mtwara
Makatibu wakuu wa Wizara (Habari, TAMISEMI, na Elimu) zilizoratibu mashindano ya UMISHUMTA na UMISSETA na Wakurugenzi wakikagua miundombiunu ya mashindano hayo kabla ya kuanza rasmi Juni 7,2021 mjini Mtwara
Na John Mapepele, Mtwara
Serikali imesema wanafunzi
sita watakaofanya vizuri mashindano ya UMITASHUMTA upande wa Riadha yanayoendelea
kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu mjini Mtwara watapelekwa katika mashindano ya
kimataifa ya Shirikisho la Michezo ya Wanafunzi Duniani (ISSF) yatakayoanza
Septemba mwaka huu nchini Slovenia
Hayo yasemwa na Mratibu wa
UMITASHUMTA na UMISSETA Taifa, Leonard Thadeo wakati akiongea na waratibu wa michezo,
makocha na walimu wa michezo kutoka mikoa yote inayoshiriki mashindano hayo
ambapo amesisitiza kuzingatia kanuni zote za michezo huu ili kuwapata wachezaji
wenye nidhamu na sifa watakaopeperusha vema bendera ya nchi yetu
“Hii ndiyo dhana ya Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ya
kutaka ufundishaji michezo kuanza kwenye shule za Awali,Msingi, Sekondari na
Vyuo ili kupata washiriki wengi walionolewa vizuri kwenye mashindano ya
kimataifa kama yanavyofanya mataifa
makubwa”. Amefafanua Thadeo
Mhe. Majaliwa alisema wakati
akifungua mashindano haya kuwa kupitia michezo na sanaa, wanafunzi watafunguliwa
vipaji vyao ambavyo vikiendelezwa vema vitawapatia manufaa mazuri ya kitaaluma na
ajira.
Katibu Mkuu wa Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt,Hassan Abbasi amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuanzisha
na kuboresha vyuo vya michezo nchini
ili kupika na kunoa vipaji vya wanamichezo na hatimaye kuviuza duniani
“Mikakati ya Serikali kwenye
Sekta ya Michezo kwa sasa ni kuhahakisha taaluma ya michezo inaboreshwa na inatolewa
kwa kiwango cha kimataifa ili wanamichezo wetu wawe kwenye viwango vya
kimataifa, tukumbuke kuwa michezo ni sayansi. “Amefafanua Dk Abbasi
Michezo ya leo kwenye riadha imehusisha mita 100 kwa wavuala
na wasichana, mita 100 kwa wenye ulemavu ambayo imefika fainali na kumalizika, mita
1500 kwa wavulana na wasichana relay mita 400×4 na mchezo wa kurusha
tufe ambao umefikia fainali ambapo mkoa wa Kigoma kwa upande wa wavulana na
Manyara kwa wanawake walishinda.